Nachukua nafasi hii kutoa shukurani zangu za dhati kutoka katika kilindi cha moyo wangu kwa Hospitali ya Kilutheri ya Hydom iliyoko mkoani Manyara kwa matibabu waliyompatia mwanangu Ally Hassan (16) aliyelazwa hospitalini hapo tokea siku ya Alhamisi Juni 13, 2013 akiwa hajitambui (in a coma) kwa muda wa siku nne mfululizo baada kuugua malaria sugu.
Shukurani maalum ziwaendee madaktari na wauguzi wote wa wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) ambao kwa siku hizo nne tulikesha nao kumuuguza Ally ambaye aliletwa hapo toka Katesh alikoenda kumtembelea mama yake wakati huu wa likizo akiwa hana fahamu. Kwa upendo, weledi na utaalamu wenu hatimaye mlifaniklwa kupambana na malaria hiyo kwa ukamilifu. Hivi sasa Ally hajambo na anaendelea kupata nafuu kila dakika.
Mama mzazi, Baba mlezi, mjomba, shangazi, mamdogo na mamkubwa mliojitoa kumsaidia Ally nawashukuru sana sana kwa upendo wenu.
AHSANTENI SANA SANA SANA.
Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Kilutheri ya Haydom sina cha kuwalipa zaidi ya kutoa ahsante kwa wote mliomshughulikia Ally pamoja na wagonjwa wengine waliolazwa hapo (nilishuhudia kwa macho yangu jinsi mlivyokuwa mkiwashughulikia wagonjwa wote kwa upendo na weledi kila dakika walipohitaji uangalizi) na kupata nafuu.
Kwa niaba ya wagonjwa wengine waliopata huduma na kupata nafuu, natoa pia ahsante kwa kazi njema, ya weledi na upendo mnaoonesha kwa kila mgonjwa anayefika kutibiwa hapo Hydom. Ninyi ni mfano wa kuigwa katika mahospitali yetu yote hapa nchini.
NAOMBA MOLA AWALIPE KWA KUWAZIDISHIA
PALE MLIPOPUNGUKIWA. MBARIKWE SANA.
AMEN
-Muhidin Issa Michuzi
Ankal akiwa Haydom na na baba mlezi wa Ally Hassan (kushoto) na mjomba
Sehemu ya mbele ya hospitali ya Kilutheri ya Haydom, Manyara
Baadhi ya wodi za Hospitali ya Kilutheri ya Haydom, Manyara
Ankal akikesha kumuuguza mwanae Ally Hassan hospitalini hapo
Ally Hassan akiwa kitandani pake akiangaliwa na mama, mamdogo, mjomba na shangazi.
No comments:
Post a Comment