Joshua Nassari |
Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ameshambuliwa na
vijana wa Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Kiongozi wa Chama cha Mapinduzi,
Mkoa wa Arusha aliyejulikana kwa jina la Kalanga na kulazimika kulazwa katika hopitali ya Selian
Mkoani Arusha katika fujo zilizotokea katika kituo cha kupigia kura cha Zaburi,
kata ya Makuyuni, Wilaya ya Monduli mkoani Arusha.
Akizungumza kutoka eneo la tukio, Mratibu wa wanawake wa
Chadema Mkoa wa Arusha Sesilia Ndossi alisema “muda wa saa 5 asubuhi tulienda
katika kituo cha kupiga kura cha Zaburi, kumsindikiza Mbunge wa Arumeru ambaye
katika Uchaguzi huo yeye alikuwa Wakala.
'lakini tulipofika hapo tulimkuta raia
mmoja mwenye asili ya kisomali akiwaita watu na kuwaambia pigia CCM, ndipo
Nassari akamuuliza kwanini unapiga kampeni kituoni, huyo Baba alihamaki,
akamrukia Nassari wakamchangia na Diwani mmoja aliyeitwa Kalanga, wakamsukuma
akaanguka damu ikaanza kumtoka puani, tukalazimika kuingilia kati na kuondoka
na Nassari akaenda mahali tulipokuwa tunalala akabadili mavazi akaenda kutibiwa
Minjingu, hata tulipofika huko
waliendelea kutufuata wakaja na gari imejaa vijana wa kimasai wakimtafuta
Nassari, hivi tulilazimika kukodi gari ambayo hawaifahamu ndipo tukamwondoa
kumpeleka Arusha hospitali ya Selian kwa matibabu zaidi'.
Taarifa zaidi kutoka Makuyuni zinasema walipomkosa Nassari
walimpiga dereva wake Gadi Palangyo na
Katibu wa Chadema wa Wilaya ya Monduli, Thomas Kilongola, hadi walipokuja
kuokolewa na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Makuyuni. Hadi tunaandika habari hii
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas hakupatikana kuzungumzia
suala hili baada ya simu yake kuita bila mafanikio.
No comments:
Post a Comment