Na Elizabeth John
BAADA ya kukaa
kimya kwa muda mrefu, mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Sajna ameachia
ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Ningekuwa single’ ambacho kimeanza
kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.
Kabla kuachia
kibao hicho, Sajna alishawahi kutamba na ngoma yake inayokwenda kwa jina la ‘Iveta’
ambayo ilimtambulisha na kufanya vizuri katika soko la muziki huo.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Sajna alisema katika ngoma hiyo, itasikika sauti ya mkali
wa muziki wa RnB nchini, Ben Pol, na msanii chipukizi C Sir Madini.
“Naamini uwepo
wa wasanii hao utanisaidie kufanya vizuri katika ngoma hiyo, kila shabiki ana
mapenzi na msanii anayemtaka yeye hivyo naamini kufuatia uwepo wapo nitajizolea
mashabiki lukuki kupitia kazi hii,” alisema.
Mkali huyo
anawaomba wapenzi wake wakae mkao wa kula kwaajili ya kuipokea video ya kazi
hiyo ambayo anatarajia kuiachia katika ya mwezi huu.
No comments:
Post a Comment