HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 08, 2013

Rais Kikwete; bado hujasikia kilio cha wapiga kura wako?



Na Bryceson Mathias
KAMA ni kudhalilika na matukio ya Mauaji ya Mabomu, Utekwaji, Uteswaji wa kung’olewa Meno, Kucha na kutobolewa Macho, Watanazania na wapiga Kura wa Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dk. Jakaya Kikwete, wamefanyiwa Unyama Mbaya na Maovu sana!
Dunia nzima imeyaona wazi maovu hayo, na imetusoma na kututazama, na ndiyo maana hata wakati Rais Barack Obama alipoingia Tanzania, gazeti la The New York Times la Marekani lilirudia kuhoji matukio ya milipuko ya mabomu, utekaji, Mauaji ya waandishi na mengine, wakimtazamisha Kikwete.
Achilia mbali gazeti la The New York Times la Marekani, hivi Rais Kikwete, sisi Wapiga kura wako, bado hujasikia kilio cha waliokuweka madarakani uwaongoze, wanaokutaka Uunde Tume Huru ya kimahakama kuchunguza ukweli wa matukio hayo?.
Rais, kama ni kudhalilishwa tumedhalilishwa kiasi cha kutosha, kama kupuuzwa tumepuuzwa kiasi cha kutosha, kama kudharauliwa tumedharauliwa kiasi cha kutosha, kama kunyonywa na kutukanwa, tumenyonywa na kutukanwa hadi na Wabunge bungeni; na Unyonge wetu ndio umetufikisha hapo!
Je, Rais kama Baba yetu, lini utatuondolea adhaa hii? Maana sasa bila aibu hata binamu zetu wanatupiga, Shangazi anatupiga, Mjomba anatupiga, Majirani nao wanatupiga, kibaya zaidi hata wapita njia, nao sasa wana uwezo wa kutupiga na hata kutukashifu. Je Rais wetu Upo? Wakemee! Wakome!.
Hivi majuzi, mtoto wa Mkulimo Waziri Mkuu Mizenga Pinda, alijikwaa na kuwapa Kiburi Polisi kupiga wanaokaidi Amri bila Shuruti, hata watoto wa Mama wa Kambo na Majirani, wameanza kutupiga wakidhani labda hatuna Baba! Mimi leo nimeamua kusemea kwako Baba, ili Uwakemee! Tutatamalizika; Utamuongoza nani?
Pinda, aliwaruhusu Polisi kuwapiga wananchi; Baba kama nilivyodai awali, leo nimeamua kusemea kwako; Sijui Kauli ya Pinda ya kutaka wanaokiuka amri ya Ma-Afande wapigwe tu! Eti Serikali imechoka, linakuingia akilini hilo?
Rais wangu, familia yetu bado ni ya Kijamaa au ya Kijangili? Kwa nini watu wafikie hatua ya kuanza kuwapiga watu, bila kufuata taratibu na Kanunii za Kisheria? Au tayari kuna watu wamebadili Utamaduni wa kuheshimiana na kujiamulia mambo yao wakidhani haupo? Je wanakufahamu ni Afande?
Nchi sasa, imekumbwa na mauaji ya kila aina, vyombo vya dola vinaua raia, matukio ya ajabu yametanda kila eneo, hadi utekaji nyara, utesaji watu lakini Mkuu wa Dola hujakohia!  Je kilio cha wapiga kura wako hujakisikia?
Kimsingi nimezoea kusikia Jogoo wakiwika kuwamusha watu kuashilia kuwa kumekucha, lakini nyakati hizi hapa nchini, nimeanza kuona hata tetea, nao wanawika, na kibaya zaidi na vifaranga navyo vimeanza kuwika; Tutafika?
 Mtoto mmoja alimuhoji Babu yake, Babuu! Hivi Kuku na yai, kipi kilianza? Baadhi ya Viongozi nchini wenye dhamana ya kuwatetea wananchi na wapiga kura wasipuuzwe wasitukanwe, wasinyonywe, wasipuuzwe, wamejishau; wakiulizwa Kuku na yai kipi kilianza, wamebaki wanacheka kama Babu.
Rushwa ikikithiri wanacheka, Ufisadi ukikomaa wanacheka, Wabunge wakitukana matusi ya Nguoni bungeni wanacheka, Watu wakiuawa na kufanyiwa vitendo vibaya wanacheka, nchi ikiporwa rasilimali zake wanacheka tu kama babu.
Ni Rai yangu kama viongozi hawa wanakusaidia Rais, kama hawakuitwa na Mungu kuwasaidia wananchi, basi maneno ya kwamba anayekubalika na wengi amekubalika na Mungu si ya kweli, ni heri kama hawakuitwa na Mungu waache kuongoza na waondoke!

No comments:

Post a Comment

Pages