HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 31, 2013

WALTER AANDAA VIDEO YA 'DORODORO'



Na Elizabeth John

BAADA ya kutamba na ngoma yake ya ‘Dorodoro’, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Walter Chilambo, anatarajia kuanza kuisambaza video ya kazi hiyo baada ya kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Walter alisema kazi hiyo ameisambaza hivi karibuni na anaomba mashabiki wake waipokee kwa mikono miwili.

“Nina imani kazi hii itafanya vizuri katika tasnia hiyo kwani mashairi yaliyopo ndani yake yamesimama na yana ujumbe kwa jamii,” alisema msanii huyo ambaye ni mshindi wa Bongo Star Search mwaka jana.

Alisema video ya kazi hiyo pamoja na ile ya ‘Siachi’ anaendelea kuziandaa na kwamba yupo katika hatua za mwisho na anawaomba mashabiki wake wasichoke kumsubiri.

“Nitatangulia kutoa video ya ‘Siachi’, nina imani itakuwa nzuri kutokana na maandalizi ya muda mrefu, najua mashabiki wanaisubiri kwa hamu ila nawaahidi hivi karibuni wataiona,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages