HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 31, 2013

'KIBABAA' YA MAKOMANDOO YAANZA KUTESA



Na Elizabeth John                               
BAADA ya kufanya vizuri na kibao cha ‘Kibega’ wasanii wa kundi la Makomandoo wameshirikiana tena na kuachia kitu kingine kinachokwenda kwa jina la ‘Kibabaa’.

Akizungumza ijini Dar es Salaam, mmoja wa kundi hilo, Fred Felix ‘Fredwayne’ alisema kazi hiyo tayari imeanza kusikika katika vituo mbalimbali vya redio na sasa wapo katika mchakato wa kuandaa video yake.

“Hii ni tofauti na ‘Kibega’ iliyokuwa inazungumzia jinsi ya kubadilisha staili ya kucheza, ‘Kibabaa’ inaelezea jinsi wasanii tunavyopishana kwa staili ya maisha pamoja n awatu wengine ambao wanaigusa jamii.

 Alisema katika wimbo huo wamehamasisha mshikamano kwa watu ambao wanafanya kazi ya aina moja, pamoja na kudumisha amani na upendo katika nchi.


Mkali huyo amewataka wapenzi wa kazi zao kukaa mkao wa kula kwaaajili ya kibao hicho ambacho kwa upande wa video kitaanza kuonekana katikati ya mwezi huu.

No comments:

Post a Comment

Pages