HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 01, 2013

ASHANTI YAFUNGA USAJILI

 Na Elizabeth John

KLABU ya Ashanti United yenye maskani yake Ilala jijini Dar es Salaam, imefunga usajili kwa wachezaji wake bila wachezaji wa kigeni wala wachezaji waliotoka klabu kubwa za hapa nchini.

Akizungumza kwa njia ya simu akiwa mkoani Kigoma, Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Abubakar Silas alisema klabu yake imefunga usajili na wanaendelea na maandalizi ya ligi kuu bara, inayotarajiwa kuannza Agosti 24.

“Swala la usajili tayari tumelifunga na kwasasa tupo mkoani Kigoma kwaajili ya maandalizi hayo, na tunatarajia kucheza mechi tatu za kirafiki tukiwa huku ili kujiweka sawa,” alisema.

Alisema katika kuhakikisha inaanza vizuri katika pazia la Ligi Kuu Bara, timu hiyo ipo katika hatua za mwisho kukamilisha taratibu za kupiga kambi nchini Burundi.

Timu hiyo ambayo imepanda daraja, itafungua pazia la ligi hiyo kwa kucheza na mabingwa watetezi, Yanga katika mechi itakayopigwa Agosti 24, mwaka huu Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaa.

 Aliongeza wakiwa nchini Burundi watacheza mechi mbili au tatu za kirafiki na kwamba mawasiliano yanakwenda vizuri na TFF pamoja na Chama cha Soka cha Burundi ili kufanikisha safari hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages