HABARI MSETO (HEADER)


September 29, 2013

MAHAFALI YA SITA SHULE YA MSINGI HERITAGE
Meneja Mkuu wa SimbaNET, Stanley Ayittah akikata utepe wakati wa ufunguzi wa darasa la kompyuta katika Shule ya Msingi, Heritage iliyopo Banana, Ukonga. Katikati ni Mkuu wa shule hiyo, Apiemi Elijah Kebaso na Mkurugenzi wa shule hiyo, Josephat Mnanka. (Picha na Francis Dande)
Mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi, Heritage, Rose Joab akiwaonesha kwa vitendo somo la sayansi, wazazi na wageni waliofika katika mahafali ya sita ya shule hiyo.
Baadhi ya wanafunzi waliohitimu mahafali ya darasa la saba wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi.
 Meneja Mkuu wa SimbaNET, Stanley Ayittah ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo akizungumza na waandishi wa habari.
Mkuu wa shule ya Heritage, Apiemi Elijah Kebaso akifafanua jambo kwa waandishi wa habari. 
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi, Heritage wakiingia kwa kwaride maalum wakati wa mahafali ya sita ya shule yao.
Macho mbeleeee...... 

Na Mwandishi Wetu

MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Heritage iliyoko Ukonga Banana wilayani Ilala jijini Dar es Salaam, Apiemi Kabaso amewataka wanafunzi kujikita katika masomo ya sayansi ili nchi iweze kupata wahandisi wa sekta hiyo.

Kibaso aliyasema hayo wakati wa mahafali ya sita ya shule hiyo ambapo wanafunzi 53 walihitimu elimu ya msingi, mahafali hayo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Alisema vijana hao wakati wakimaliza ahatua ya kwanza, watambue kuwa taifa lina kabiriwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa wataalamu wa sayansi, hivyo wanalo jukumu la kulinasua taifa kwa kusoma kwa bidii masomo hayo.

Aidha, kwa kulitambua hilo, ndio maana shule hiyo imeamua kuwekeza zaidi kwenye masomo hayo ya sayansi ambapo kwa sasa wamefungua ntanet ambayo itawasaidia wanafunzi katika masomo yao.

“Tunaishukuru kampuni ya SimbaNet kwa msaada wao wa kuwfungulia Intenet, kwani wanaamini itawasaidia katika kumiza ndoto za wanafunzi katika kujitafutia taarifa mbalimbali za masomo”alisema.

Aliongeza kuwa watakuwa waangalifu katika matumizi ya internet hiyo ili kudhibiti matumizi yasio sahihi kwa wanafunzi.

Naye Meneja Mkuu wa Kampuni ya SimbaNet Stanley Ayittah, alisema kampuni yake ilitoa kompyuta hizo kutokana na mfumo wa sasa kutawaliwa zaidi na sayansi na teknolojia.

Aidha, alivutiwa na mazingira ya shule hiyo kwani  ni rafiki na yanamfanya wanafunzi apende kujisomea ambapo pia aliwataka wanafunzi hao kuepukana anasa na vishawishi vya dunia ili wafike mbali kielimu.

No comments:

Post a Comment

Pages