Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI Serikali ya Mtaa
Luguluni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam Saidi Mahadula, amesema mtaa huo haujabahatika kupata shule ya msingi tangu ulipoanzishwa 14 iliyopita.
Mahadula alitoa kauli hiyo
kwenye mkutanoa wa hadhara uliyokuwa na lengo la kujadili maendeleo na kero za
mtaa huo, uliofanyika kwenye viwanja vya Dk Halid, Makondeko jini jana.
Alisema kutokana na
kukosekana kwa shule katika mtaa huo, watoto hulazimika kusafiri umbali mrefu kwa
ajili ya kufuata shule jambo ambalo wakati mwingine kuwa la hatari kutokana na
baadhi ya watoto kuwa na umri mdogo.
Mahadula, aliyataja maeneo
ambako watoto hao wamekuwa wakifuata shule kuwa ni Mbezi Luis, Kibamba,
Mpijimagohe na Mshikamano.
“Umefika wakati wa
kuunganisha nguvu zetu na tushirikiane ili kwa pamoja tuweze kumaliza kero inayotukabiri
pamoja na watoto wetu ambao tunawatarajia hapo baadaye wajekuwa wataalamu
wetu”alisema Mahadula.
Aidha, ilikufikia adhima ya
kumaliza tatizo hilo, wakazi hao kwa pamoja wamekubaliana kuanzaisha mchakato
wa kujenga shule kwa kuanzisha kitu walichokiita Dira ya maendeleo (mfuko).
Mahadula lengo la dira hiyo
ni kutafuta fedha kutoka Manispaa ya Kindoni, Serikali Kuu, wafadhili wa ndani
na nje ya nchi, kampuni za simu,wadau mbalimbali na wakazi wa mtaa huo.
Mkutano huo pia ulijadili
kero mbalimbali ikiwemo maji amayo inaonekena kuwa kilio cha taifa pia kulikuwa
na ile ya kusimamishwa ujenzi wa mnara wasimu za mkononi Tigo kwa madai kuwa
mionzi ya mnara huo ungesababisha madhara ya kiafya kwa wakazi hao.
Hata hivyo, kero ya mnara
huo ilipatiwa ufumbuzi baada ya serikali kumtuma Ofisa mshauri wa mazingira, kwenye
mkutano huo, aliyewahakikishia wakazi hao kuwa sheria zote za ujenzi wa mnara
huo zimezingatiwa hivyo hakutakuwa na madhara yeyote katika afya zao.
Kutokana na kauli hiyo
wakazi hao walikubali kampuni hiyo iendelee na mchakato wake wa kumalizia mnara
huo ambao utasaidia kuwa sogezea maendeleo kwa kuwafikishia huduma ya umeme
wananchi wa eneo ulikojengwa.
No comments:
Post a Comment