HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 12, 2013

Q CHILLAH AIBUKA NA 'SINDANO ZA MASAA'



Na Elizabeth John


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Abubakar Shaaban 'Q-Chilla', anatarajia kuachia kazi yake mpya hivi karibuni inayokwenda kwa jina la ‘Sindano za Masaa’ hivi karibuni.

Q Chilla hivi sasa anatamba na kibao chake cha ‘Beautiful’ ambacho kinafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio kutokana na ubora wa mashairi yaliyopo ndani yake.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Q Chilla alisema kuwa maandalizi ya kazi hiyo yapo kwenye hatua za mwisho na muda wowote ataisambaza katika vituo mbalimbali vya redio.

Chilla alisema hawezi kuweka wazi ni lini ataisambaza ila anawataka mashabiki kukaa mkao wa kuipokea kwani ipo katika hatua za mwisho za kukamilika.


“Naomba wapenzi wa kazi zangu wakae mkao wa kula kwaajili ya kazi hii ambayo naamini itakuja kufanya vizuri kutokana na ubora wa mashairi ya wimbo huo ambao utakuja kuliteka soko la muziki huo,” alisema.

No comments:

Post a Comment

Pages