HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 12, 2013

'ROHO' YA RICH MAVOKO MBIONI KUTOKA



Na Elizabeth John
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Richard Martin ‘Rich Mavoko’ anajipanga kuachia ngomayake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Roho Yangu’ ikiwa ni mfululizo wa kuwapa burudani mashjabiki wa kazi zake.

Rich Mavoko, kwasasa anmatamba na kibao chake cha ‘Mapenzi ya sasa’ licha ya kuwa na kazi nyingi ambazo zilimtambulisha na kufanya vema katika soko la muziki huo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mavoko alisema kazi hiyo anatarajia kuanza kuisambaza wiki ijayo katika vituo mbalimbali vya redio na anaomba wapenzi wake wakae mkao wa kula.

 “Video ya kazi hii natarajia kuifanya Afrika Kusini, kutokana na maudhui ya wimbo huo ikiwa ni pamoja na kutafuta mazingira ambayo yanavutia kurekodi, naomba wapenzi wangu mnipe sapoti katika hili,” alisema.


Licha ya kuwa mchanga katika soko la muziki huo, Rich Mavoko amesambaza kazi zaidi ya tano na zote zimefanya vizuri kutokana na staili ambayo anaitumia katika kazi zake kuliteka soko la muziki huo.

No comments:

Post a Comment

Pages