HABARI MSETO (HEADER)


October 14, 2013

Chadema kuikaba koo CCM na kuigalagaza Dodoma
Na Bryceson Mathias
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Dodoma, kinakusudia kukikaba Koo na kukigalagaza Chama cha Mapinduzi (CCM), katika kuziba nafasi ya Udiwani Kata ya Mpwayungu wilayani Chamwino Manispaa ya Dodoma.
Kata hiyo iko wazi kutokana na Kifo cha aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chamwino, Laurent Hoya, aliyefariki ghafla, 16.8.2013, ambapo Mgombea Mtarajiwa ni ndugu na Hoya (mtu na Mdogo wake), kwa wazazi wao.
Chadema itamuweka, Josiah Samwel Mtonyi, Mhitimu wa Bachelor of Rural Development 2008-2011 Sokoine University of agriculture Morogoro, ambaye amemthibitishia Mwandishi ni ndugu na Hoya na kwamba ameweka nia Kugombea nafasi hiyo toka moyoni si kwa kushawishiwa.
Mgombea Mtarajiwa Mtonyi, aliwashauri Wazazi na wananchi wa Kata ya Mpwayungu waliomlea toka Utoto, kuachana na Imani potofu kuwa kwa kugombea nafasi ya Hoya anafurahia Kifo chake, ila anauenzi uongozi wake na kazi aliyoifanyia Jamii na Familia.
Alisema, Mwananchi na Ndugu asiyemuenzi Hoya, ni yule ambaye hatamuunga Mkono yeye anayekusudia kuuenzi uongozi wa Hoya usipotee katika Jamii na familia, kama walivyofanya Watoto wa Nyerere, Kawawa, Karume, Kigoma Malima, Makamba na wengine waliohai”.alisema Mtonyi.
Mtonyi alipoulizwa kwa nini kwa elimu yake asigombee Ubunge alisema, hata alipokuwa akilelewa alianza kunywa Maziwa, Uji na hatimae Chakula Kigumu kwa maana ya Ugali, Kande na Vyakula vingine; Hivyo anautaka Udiwani awajenge wananchi vizuri kiuchumi na kisiasa.
Aidha Mwenyekitu wa Chadema Kata ya Mpyayungu, Joab Mtachi, wananchi na aliyekuwa Mgombea wa Udiwani wa Kata hiyo kwa tiketi ya Chadema 2010, Aloyce Zamoyoni, wote wanamkubali na kumuunga Mkono ingawa hawaamini masikioni mwao maamuzi ya msomi huyo kuwatumikia wananchi ngazi ya Kata.

No comments:

Post a Comment

Pages