Na Bryceson Mathias, Mvomero
KWA mara nyingine, Wakulima wa zaidi ya 100 wa Kata ya Hembeti wilayani Mvomero, wamefunga barabara ya Turiani, Morogoro, Dar es Salaam na Tanga, wakiidai Serikali iwarejeshee Bonde lao la Mpunga la Mgongola lenye Mgogoro wa mapigano ili walilime, huku wakimjeruhi usoni kwa mawe Diwani wa CCM Kata ya Hembeti, Juma Malaja.
Akizungumza na mwandishi toka mafichoni, Mlinzi wa Amani na Mtendaji wa Kata Hembeti Henry Kabuye amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo, ambapo magari zaidi ya 10 yakiwepo ya abiria na mwandishi akiwemo, yalikwama kijijini hapo.
Kabuye alisema, tayari ametoa taarifa kwa vyombo husika akiwemo OCD wa Wilaya KAmanda Emanuel Gariamoshi na Mkuu wa Wilaya Antony Mtaka, tayari kwa kumaliza tatizo hilo ambalo ni la muda mrefu sasa.
Wakati Mwandishi anaendelea kufanya juhudi za Makusudi kuwasiliana na Viongozi hao, Wakulima hao waamesema, Serikali imekuwa haiwatendei haki kwa kutotoa ufumbuzi wa kudumu dhidi ya mapigano baina yao na wafugaji, ambapo vibanda mashambani mwao vilichomwa.
Hii ni mara ya pili kwa siku za hivi karibuni ambapo wananchi wa vijiji vya Kisala na Kwamtonga Kata ya Sungaji wilayani humo, walifunga barabara hiyo baada ya wafugaji kulisha Shamba la Mahindi Eka tatu za Alex Kazimheza, ambapo wakulima kwa Hasura walikatakata kwa Mapanga Ng’ombee zaidi ya 15.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mtaka, aliwapa siku 7 Wafugaji kuhama kwa hiari na siku 14 kuhama kwa lazima na kuwatia faini Mil.7/-, jambo ambalo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Sungaji, Musa Kombo, amebeza akisema siku 7 za Mtaka zimekuwa siku 70 za kuwasumbuaa wakulima.
Aidha Polisi toka wilayani Mvomero walifika Hembeti ‘Shorcurt’ eneo la tukio la wakiungana Askari waliotoka Mtibwa na Turiani lakini kila walipopiga Mabomu kuwatawanya wananchi waliojipanga kwenye daraja, wao walichota maji na kunawa nyuso hivyo polisi, kurejea ili kutafuta nguvu ya ziada, lakini hadi saa Sita hali ilikubado tete.
Wakati huo huo wananchi wenye Hasira wamemjeruhi kwa Mawe usoni Diwani wa Kata ya Hembeti, Juma Malaja, kutokana kile walichodai alikuwa akiongea na Polisi ili wawashambulie kwa mabomu na kuwatoa eneo husika. Mwingine aliyejeruhiwa ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Dihombo, Pantareo Mathias,ambaye naye amepopolewa mawe usoni.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Antony Mtaka alipojaribu kwenda kutoa suluhu ya Mgogoro huo ili aweze kuzungumza na wakulima, wakulima hao wakiwa na hasira walilipopoa Mawe Gari lake na la Mkurugenzi wa Wilaya ya Mvomero, Wales Karia, na kulazimika kurudi kutafuta njia ya ufichoni ili kuwafikia wananchi hao.
No comments:
Post a Comment