‘Sikio la kufa halisikii dawa’
Na Bryceson Mathias
KAULI ya Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki kwamba Majangill wai waue ni itamgharimu na kukipata kama kile kilichompata Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda, pale aliposema wauaji wa Albino naowauawe.
Waziri Kagasheki alisema hayo hivi karibuni Mjini Arusha, baada ya kuongoza matembezi ya kupiga vita ujangili wa tembo yaliyoandaliwa na Taasisi ya David Sheldrick Wildlife Trust kupitia kampeni ya meno ya tembo..
Kagasheki alisema, “Wana usalama wakikutana na majangili huko kwenye porini wawamalize huko huko, tena katika jambo hili nawaomba wale watetezi wa haki za binadamu wafunge midomo.
“Hata hao majangili wakiwakuta watawamaliza pamoja na tembo,” alisema Kagasheki huku umati wa watu uliokusanyika ukipiga makofi”.
Alisema kuwa kazi ya serikali ni kuwatetea wale wasio na uwezo wa kujitetea wenyewe kama wanyama wa porini akiwemo tembo na kwa kuwa kumekuwa na tatizo la kesi kuchukua muda mrefu, suluhisho ni vyombo vya ulinzi kumalizana na majangili huko huko pindi wakiwakamata
Ingawa Kauli ya Kagasgeki ina nia nzuri ya kuwatia hofu majangili wasiue tembo, ambayo ni swan a ile ya Waziri Mkuu kwa Wauaji wa Albino, ninachofahamu itabadilika na kumliza kama ilivyomliza Pinda alipolazimika kuomba hisani kwa machozi bungeni, kwamba hakuwa na maana iliyotafsirika.
Waswahili wana msemo usemao ‘Sikio la Kufa halisikii dawa’. Baada ya Pinda kuonja Joto ya Jiwe kuhusu wauaji wa Albino nao wauawe na kusamehewa kuwa hakusema kwa kukusudia kama ilivyotafsirika, lwa bahati mbaya baadaye alijikwaa tena aliposema watu wasiotii amri ya Polisi bila shuruti , Piga tu!.
Pamoja na kwamba Kagasheki ametanguliza Silaha ya Maombi kwa watetezi wa haki za binadamu wafunge midomo dhidi ya kayli yake kuhusu kutetea wa Ujangili.
Bado naamini silaha hiyo ya Kagasheki, haitamsaidia kama ambavyo Pinda haikumsaidia na ndiyo maana sasa hivi watetezi wa aina hiyo wameamua kumshitakiwa mahalamani kwa kauli hiyo aliyoitoa bungeni humo humo ya wasiotii amri ya polisi, ‘Piga tuu’.
Wananchi mkoani Morogoro waliohojiwa na Wandishi na Radio za Kijamii, Wamepinga Kauli ya Serikali kupitia kwa Waziri Kagasheki kwamba, Wana Usalama wakikutana na Majangili wamelizane.
Mmoja wa wachabiaji alisema, Kauli hiyo atasababisha hata Wakulima wanaokwenda mashambani wakiwa na Panga, watadhaniwa ni Majangili hivyo watauawa hata kama hawana Hatia.
Mchangiaji mwingine alisema, Wanaosafirisha na kufadhiri Ujangili ni hao hao Vigogo wa Serikali, kwa nini Kagasheki asiwaanze hao akakimbilia kuwaambia walalahoi? Alisema, inaonesha Kagasheki ameshindwa wajibu wake wa kutafuta mbinu mbadala.
Mchangiaji mwingine ambaye aliuunga Mkono na kupingwa na wananchi wengi waliochangia alisema, “Kama sheria zilivyo kwa wenzetu wenye kuzitekeleza bila kuweka siasa, Mtu akibainika akatwe Mkono, na akirudia akatwe Mkono mwingine, na akiongeza auawe!
Ni rai yangu Serikali itafute njia mbadala ya kuhakikisha, watu wanaohisiwa kufadhiri utoroshaji na Ujangili wa Tembo na rasilimali za nchi hii, basi wasiwe ndio wale ambao wanasimama majukwani na kuwakataza watanzania kile ambacho wao wanafanya.
Utamaduni wa usafi na uadilifu ukianzia nyumbani, kwenye familia, majukwani, Maofisini, na popote pale, ni dhahiri watu watajifunza kutofanya makosa na matokeo yake watakuwa wadilifu kama viongozi walivyo kwenye nafasi zao!
nyeregete@yahoo.co.uk 0715933308


No comments:
Post a Comment