Na Bryceson Mathias
UMATANO 11, Septemba
2013 nilisema katika Makala yangu juu ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Katiba na Sheria, Pindi Chana, kwamba kutokana na kinachoonekana kuwa mwavuli
wake wa kukifunika Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukivusha katika mchakato wa
mapendekezo ya Katiba Mpya! Si tu umetoboka! Bali Umechanika.
Haikuwa tu Chama cha
Alliance for Democratic Change (ADC) kupitia kwa Mwenyekiti wao, Said Miraji,
kumshushua Chana na kuutoboa Mwavuli huo au Chama cha Wananchi
(CUF), bali hata mimi, kwa kauli yake haikuwa sahihi nilimmtaka atuombe radhi
watanzania, lakini alijibaraguza na kukaa kimyaa!
Hivi ni lini viongozi
wetu watafikia kuwa na uadilifu ili wanapofanya madudu kama aliyofanya Chana!
Alipotutumainisha na kujigamba mle mjengoni kuwa wazanzibari wameshirikishwa
kuhusu Mchakato wa Mapendekezo ya Katiba Mpya, kumbe sivyo?
Ingawa kwa kauli za
Viongozi wa Juu wa Serikali zote mbili inaonesha wazanzibari walishirikishwa.
Wazanzibari wenyewe wakiwemo ADC na CUF walikataa katu katu, na kudai kitendo
kilichofanywa hakina udugu wala kuaminiana isipokuwa kudharaulina.
Watanzania sasa
wanayo kila sababu kumhoji Chana, nini dhamira yake kusema walishirikishwa
wakati hawakushirikishwaa? Wananchi wana fursa kutilia shaka nia za baadhi ya
Viongozi hadi kufikia kubadilisha yale yaliyokubaliwa kwa pamoja na Vyama vya Upinzani
wakiwepo.
Katika hilo Watakuwa
wana haki ya kuuliza nia ni hii yetu sote ya kupata katiba mpya kwa kutumia
njia za kikatiba na kisheria au wana dhamira nyingine iliyojifisha nyuma ya
kuweka kile ambacho hakikukubalika kwenye maridhiano ya pamoja?”
Nafarijika na Kauli
ya Rais Jakaya Kikwete aliyosema bila kumung’unya maneno “Hivyo basi napata
tabu kuyaelewa madai kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haikushirikishwa
msingi wake nini! Labda kuna kitu sikuambiwa,” alisema.
Alisema aliulizia
kuhusu hoja ya kamati kutokufanya vikao Zanzibar kusikiliza maoni ya wadau,
akaambiwa kuwa kanuni za Bunge hazina sharti hilo, hivyo kamati haistahili
kulaumiwa.
“Kama hivyo, nashauri
kuwa suala hili lirudishwe bungeni ili wabunge walizungumze na kulifanyia
uamuzi muafaka. Vinginevyo watu wataendelea kulaumiana isivyostahili,” alisema.
Mimi huwa inanipa
tabu pale ninapoona mtu wa kutegemewa na elimu kubwa, ambaye wananchi katika
eneo alipo wangetaka awaongoze kwa kushindanishwa na wengine, halafu anafanya
kitu cha kuwashangaza na kuwasikitisha watu.
Kule kwetu Njombe
ikitokea mtu huyo kafanya jambo ambalo watu wamelipinga hadi likafika kwa
Kiongozi wa ukoo alikapinga katika maamuzi yake, mtu huyo huwa hawezi hata
kufika msibani, kwenye sherehe au kwenye mkusanyiko wa kijamii kwa
sababu kwa aibu hunekana msaliti.
Sasa Mkuu wa Kaya
kaurudisha Mjadala wa mapendekezo ya Katiba mpya bungeni ukajadiliwe kutokana
na kuona mapungufu aliyoyaainisha. Je wenzangu na mimi mlioushupalia kama
mnatengeneza Katiba ya Vyama vyenu mna nguvu? Mimi huwa nampongeza sana Mstaafu
Rais, Ally Hassan Mwinyi, na Dume la Mbegu ya Maamuzi Magumu, Edward Lowasa!
Hali ingefika kama
hapo ilipofikia pa kuonekana kulikuwa na kukosekana kwa kauli za usahihi kama
alivyofanya Chana, wangefanya maamuzi magumu! Lakini siku hizi watu hao hatuna
serikalini na bungeni, isipokuwa wapo wanaowalazimisha ng’ombe wapure maji wao
aaa!!
Hatutafika, tunataka
nao wawe na uadilifu wa uwajibikaji wanapofanya madudu ya wazi kama uposhwaji
wa mapendekezo ya katibaa mpya ulivyokuwa bungeni.
nyeregete@yahoo.co.uk 0715933308


No comments:
Post a Comment