HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 10, 2013

SEREKALI IMEANZA KUPAMBANA NA DAWA FEKI ZA MIMEA

Mahmoud Ahmad, Arusha

Serekali na wadau wa chama cha watengenezaji,waagizaji na wasambazaji wa dawa za mimea na mbegu hapa nchini(CROP LIFE TANZANIA)wameanza kupambana na uingiuzaji wa dawa feki za mazao katika kuongeza thamani ya mazao na kipato kwa mkulima hapa nchini.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa chama hicho hapa nchini Harish Dhutia wakati alipokuwa akiongea na wanahabari kwenye semina ya siku mbili kwa wadau hao pamoja na mwakilishi wa wizara ya kilimo na chakula na mkurugenzi wa TPRI.

Dhutia alisema kuwa kumekuwapo na ongezeko la madawa feki kwenye soko la bidhaa hizo hapa nchini kiasi kuwa kumekuwa kukiwanyima wakulima ongezeko la thamani ya mazao na kipato hivyo wameamua kuanzisha mapambano hayo kudhibiti uingizaji wa dawa feki.

“Unajua udhibiti wa dawa feki za kilimo unahitaji ushirikiano kati ya wadau na serekali na hasa matumizi sahihi ya dawa za kilimo katika kukuza mimea na tusiposhirikiana tutashindwa kufikia malengo ya serekali ya matokeo makubwa sasa katika sekta ya kilimo”alisema Dhutia.

Aidha mwenyekiti huyo alitanabaisha sasa kumekuwepo na matumizi ya vifungashia vya dawa na wakulima wamekuwa wakivitupa ovyo kiasi cha kuharibu mazingira na kuongeza sumu mbalimbali kwenye maeneo yao na kuwa hatari kwa afya za binadamu na mimea hvyo kampeni hii itakwenda sambamba na kutoa elimu kwa wakulima hapa nchini.

Kwa upande wake mkurugenzi wa TPRI alisema kuwa serekali na sheria za kudhibiti ongezeko la dawa feki imekuwa ni tatizo kwao kwani bajeti yao imekuwa finyu katika kudhibiti suala hilo na kuomba serekali kuongeza bajeti ili nao waweze kuingia kwa undani kwenye kudhibiti dawa feki hapa nchini.

Akatanabaisha kuwa serekali ipo makini kwenye suala hilo na kuwa mipango ya kuongeza ongezeko la chakula ipo kwenye mpango wa matokeo makubwa sasa unaoendeshwa na serekali hii ni moja ya vipaumbele vya serekali.

Hapa umeona tunaanza na udhibiti wa vifungashia vya madawa hususani makopo ya dawa kwani yamekuwa yakiharibu mazingira na ni sumu kwa binadamu kama hayatawekwa katika mpangilio na kuyaharibu itakuwa tunafanya kazi bure kwenye sekta ya kilimo ambayo ni muhimili wa uchumi wa taifa hili.

No comments:

Post a Comment

Pages