Na Bryceson Mathias
WAKATI Mbunge wa Kahama, James Lembeli (CCM), akiibana Koo Serikali iache tabia ya kuvifungia vyombo vya habari, wananchi waliotoa maoni yao kuhusu kufungiwa kwa vyombo vya habari kila mara wamesema, sasa watalishwa Utapiamulo wa Habari.
Lembeli akipinga tabia hiyo alisema, mara zote vyombo vya habari siku zote ndivyo vimekuwa watetezi wa wanyonge. Hivyo ukitaka kujua au kuona Serikali yenye dalili za kuelekea kubaya, huanza kwa kufungia au kudhuru vyombo vya habari na halafu binadamu.
Wa kwanza kutoa maoni alikuwa ni Mkulima wa Mpunga na Mazao ya Biashara mkoani Morogoro, Azaria Shola, ambaye alisema, Kitendo cha Serikali kuyafungia magazeti yanyowasemea wasio na Sauti (Voiceless), ni sawa na kuwalisha habari zenye Utapiamulo.
Shola alisema, wao kama wakulima wamekuwa wakipewa mchango mkubwa na utetezi wa vyombo vya habari ambapo alisema, hivi Mawakala wa Mbolea na Pembeo wamekuwa wakiwasambazia Mbole na Pembejeo Feki, lakini mchango wao kilio chetu kimesikika.
“Tumekuwa tukitozwa Kodi ya mazao yetu tukitoa mashambani kwenda nyumba kwenye vizuizi vyenye kuwanufaisha watu binafsi, lakini kwa utetezi wa vyombo hiv kimesikika.
“Tumekuwa tukitozwa Kodi ya mazao kwenye vizuizi tukitoa mashambani kwenda nyumbani tukiwanufaisha watu binafsi, lakini kwa utetezi wa vyombo hivyo tabia hizo zimekoma, maana tulikuwa kama tunawalimia wao, tunaacha magunia hapo, na wao kuwa matajiri kuliko sisi.”
Shola alisema, kwa yeye ambaye anajua msaada wa vyombo vya habari, ukivifungia vyombo hivyo kwake ni sawa kumfanaya awe na kuwashakoo ya habari maana unamlisha hari zenye utapiamulo kwa maana zisizo na ukweli na mashiko ya hali halisi ilivyo kwenye Jamii.
Mhadhiri mmoja wa Mzumbe aliyetaka asitajwe jina alisema, Kitendo cha kuvifungia vyombo vya habari vyenye kuthubutu kusema kile kinachodhaniwa ni siri za serikali wakati hakuna siri, ni sawa na mazazi anayeamua kwa makusudi kumlisha mwane chakula kisicho na virutubisho ilihali akijua madhara yake.
Tunafahamu ili mtoto ajengeke kifikra, kiafya, kiakili na kimaumbile ni lazima ale vyakula vya Vitamini zote mihimu, Vyakula vya Wanga na kujenga Mwili Mwili, sasa kama tunao kwa kusudi mtu mwenye uelewa anakengeuka kwa makusdi basi ana shida kubwa.
Mfugaji wa kimasai ambaye amewahi kuwa Kiongozi hadi kwenye Ngazi za Uenyekiti na Udiwani wilayani Mvomero na kukataa jina lake lisitajwe alisema,
“Kwa kuyafuta na kuyafungia magazeti ambayo yanawapanua wananchi kimawazo, ni kuwataka wabaki mbumbu ili wasiangalie mbali, na matokeo yake inataka wawe wanadhulumiwa wasipate akili hata ya kudai haki zao zinazoporwa na wenye kusudi hilo”.
Aidha Mwanamke pekee aliyezungumza na Mwandishi wa Makala hii toka Gairo Hospitali ya Misheni ya Belaga kijijini alisema, “kuyafungia magazeti ambayo yanafika hadi kijijini kuona tunavyozalia kwenye miembe, sakafuni, kwa wakunge wa kienyeji wasio hata na ujuzi ni kutuhatarishia maisha.
“Kwa elimu tunayoipata ndani ya magazeti, vyombo vya habari vya jamii, inatusaidia tuondokana na uelewa wa Adamu na Hawa, badala ya kutumia sili za uzazi wenye hatari sasa hivi tumeanza kufumbua na kutumia vifaa vya kisasa visivyo madhara ya magonjwa”.
Alihoji, Kwa nini ipo Mahakama na kushitakiwa na Jamhuri? kijiji mwananchi akiharifu anapelekwa kwa nyumba 10, akishindikana anaenda mbele, mbona Serikali haifanyi? Inataka tufanye yenyewe isifanye?
nyeregete@yahoo.co.uk 0715933308.


No comments:
Post a Comment