![]() |
Mmoja wa
wakulima wa Mpunga (kulia)
akimuonyesha
Mpunga uliomo shambani Mkuu wa
Mkoa wa
Morogoro, Joel Bendera wa Pili Kushoto.
|
WAKULIMA wa Mpunga, Mahindi na Mazao mengine wa Kata ya Dakawa na Maeneo mbalimbali wilayani Mvomero, wamelalamikia kitendo cha Mawakala wa Mbolea na Pembejeo, kuwasambazia Mbolea na Pembejeo feki, zinazoua mazao yao kupitia mfumo wa Vocha.
Wakihojiwa na Radio Abood mwanzoni mwa wiki, wananchi hao pia wamelalamikia Ujazo mdogo wa Mbolea na kuwa kinachosikitisha, mara kadhaa Mbolea hiyo ikiwekwa kwenye mazao imekuwa ikiua mazao, kuyadumaza, kubadilidha rangi na hatimae kuharibika.
Mbali ya mbolea hiyo kuwa Feki na iliyopungua Ujazo, wakulima hao wamesema, kwa uzoefu walionao wanaona mbolea hiyo imepungua au kukosekana Virutubisho vyake 13 muhimu, na ndiyo maana inawafikisha kuwafanya maskini wa kipato na kuwasababishia njaa.
Wakulima wa Vijiiji vya Kibindu na Mziha Kata ya Kanga waliotoa michango walidai, wao wana Mbolea ambayo imetelekezwa na kwa athari iliyojitokeza wanaona hawawezi kuitumia na imebaki kwa viongozi wao ikiwa haina kazi.
“Ni heri tuachiwe kununua mbolea wenyewe hata ikiwa aghali kiasi gani tunaijua mbolea nzuri na Feki hivyo tutachambua ipi feki, ipi nzuri kwa ajili ya mazao yetu, la sivyo tukicheza na nyani kwa kupenda vya bure tutavuna Mabua” alisema Mkulima mmoja wa Dakawa.
Mawakala wa Pembejeo mbalimbali waliohojiwa na gazeti hili wilayani Mvomero, wamekanusha kuhusika na athari hizo, na hata walipoonyeshwa Upungufu wa Ujazo na uharibifu wa Mazao, bado walikanusha kuhusika wakidai ndivyo vilivyo toka kiwandani.
Mkuu wa Mkoa Morogoro, Joel Mkaya Bendera, alikiri kupokea Malalamiko ya Wakulima wa amekubaliana nao kuwepo usahihi wa malalamiko hayo na kusisitiza kwamba, Mawakala wanatakiwa kuwa makini kuhakiki Ujazo na Ubora wa Mbolea, wakati serikali ya Mkoa ikilifanyia kazi suala hilo.



No comments:
Post a Comment