HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 29, 2013

AMUUA MPENZI WAKE KWA WIVU WA MAPENZI
Na Datus Boniface, Jeshi la Polisi, Iringa

MKAZI wa kijiji cha Migori Iringa,  Alex Sihayo (38) amemchinja kwa kumkata koromero na kumua mwanamke nayedaiwa kuwa ni mpenzi wake kisha na mwenyewe kujiua kwa kunywa sumu.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Ramadhan Mungi (pichani), alisema mauaji hayo yamesababishwa na wivu wa mapenzi.

"Mauaji yametokea Desemba  27,ambapo mwanaume huyo ambaye kwa sasa ni marehemu  alitenda mauaji hayo kwa kumchinja mpenzi wake Anna Mpinga (30), na kutenganisha koromeo na kiwiliwili na kisha kumfunika marehemu na blanketi kitandani" alisema Kamanda Mungi.

Aliendelea kufafanua kwamba,  marehemu alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke huyo kwa muda, mara baada ya kuachika kwa mumewe, lakini mahusiano ya marehemu hao  yalitaliwa  na ugomvi wa mara kwa mara.

Kwa mujibu wa Kamanda Mungi, mara kwa mara marehemu  alikuwa akimtuhumu mpenzi wake kutokana kutokuwa mwaminifu kipindi cha uhusiano wao.

Alifafanua siku ya tukio hilo, wakiwa chumbani  kabla ya kujiua kwa sumu, alimchinja mpenzi wake kwa kumpitishia kisu shingoni na kukata koromeo na kuhamia sehemu ya kinywa na kumkata sehemu ya mdomoni hadi usawa wa taya.

Aliongeza kuwa mara baada ya kumaliza unyama huo  aliufunika mwili wa marehemu na kuacha ujumbe unaosomeka "NImemchinja mwenyewe nimemwambia aache umalaya" kisha  kutokomea mtaani.

Hata hivyo, mwanaume huyo akiwa mtaani alikunywa pombe aina ya Vodka kisha kunywa sumu na kujiua.

Aidha, miili ya mwanamke huyo na mpenzi wake  iligunduliwa na majirani,na wasamalia wema  na baadaye kutoa taarifa  Polisi.

Alisema miili yao umezikwa katika makaburi ya kijijini hukuuchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

No comments:

Post a Comment

Pages