MAMIA ya wakazi wa jijini Dar es Salaam leo, wamejitokeza
kwa wingi katika kumsindikiza gwiji wa vichekesho nchini, Said Ngamba ‘Mzee
Small’ katika safari yake ya mwisho, ambako alizikwa jana jioni katika makaburi
ya Segerea jijini Dar es Salaam.
Aidha, Rais Jakaya Kikwete, alifika nyumbani kwa marehemu
Tabata, kuwapa pole wafiwa, ndugu, jamaa na marafiki.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa maziko, Muigizaji
mkongwe, Bakari Mbelemba ‘Mzee Jangala’ alisema Mzee Small ni mfano wa kuigwa
katika tasnia ya uigizaji na wataendelea kumkumbuka na kumuenzi, huku akiwaasaa
wasanii chipukizi kuiga mazuri yake.
Naye Rais wa Bongo Movies, Steve Nyerere, alizidi kuwaasa
wasanii vijana kupenda na kufuata nyazo za wakongwe hao tofauti na hali ilivyo
hivi sasa, ambako chiku na dharau zimekuwa zikitawala.
Steve alikwenda mbali zaidi na kudai, kifo cha Mzee Small kimewaweka
kwenye hali ngumu, kwani wakati akiugua, wasanii wa Bongo Movies walikuwa
wazito kumjulia hali na hata kutoa msaada, jambo wanalolijutia.
Mzee Small aliyezaliwa mwaka 1955 katika Kijiji cha
Kililima, Kilwa mkoani Lindi, alifariki dunia Juni 7 katika Hospitali ya Taifa
Muhumbili alikokuwa amelezwa.
Ngugu jamaa na marafiki wakishiriki mazishi ya msanii wa maigizo, vichekesho marehemu, Said Ngamba maarufu kama mzee small katika makauri ya Segerea jijini Dar es Salaam, leo.
Baadhi ya
waombelezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa msanii wa
Maigizo ya Vichekesho, Said Ngamba ‘Mzee Small’ wakati wa kuelekea kwenye
makaburi ya Tabata Segerea jijini Dar es Salaam.
Safari ya mwisho ya mzee Small.
Mazishi ya mzee Small.
No comments:
Post a Comment