TIMU ya soka na kituo
kikuu cha mabasi Mkoani Mbeya Terminal FC juzi ilifanikiwa kuondoka ka kitita
cha shilingi 100,000/ baada ya kuibugiza bila hurumu timu ya Ghana FC ya jiji
hapa kwa mabao 4-2 katika mchezo wa ngao ya hisani ikiwa ni ufunguzi wa ligi ya
Malafyale Interteiment Cup.
Katika mchezo huo ilikuwa wa aina yake kutokana na timu hizo
kuwa na upinzani wa jadi ulifanyika katika uwanja wa shule ya Msingi Mbata,
Ghana ndiyo waliokuwa wa kwanza kuliona lango la wapinzani wao kwa kupitia
mchezaji wao Frank Matiga dk 25 ya
mchezo.
Hata hiyo Termina FC walikuja na kwa kasi kujibu mashambulizi
na kabla ya kwenda mapumziko walikuwa wamesha pachika magoli mawili wavuni kupitia
kwa Hassan Mwainongi dk 34 na 40 amabapo
hadi mapumziko Termina walikuwa Mbele kwa 2-1.
Kipindi cha pili kilianja kwa kasi huku timu zote
zikishambuliana kwa zamu lakini bado jaazi la Ghana FC liliendelea kuzama kwani
dk ya 70 Eliud Michael aliiandikia bao la tatu timu yake huku bao la nne
likiwekwa kimyani na mchezaji Bryton Mponzi dk 90 ya mchezo wakati goli la pili
la Ghana FC likifungwa na Said Abdalah dakika za lala salama.
Akizungumza na kabla ya Mgeni Rasmi kukabidhi zawadi
Mkurugenzi wa Malafyale Interteimnt Charlesi Mwaipopo waandaaji wa ligi hiyo alisema
kuwa sababu za kundaa mashindano hayo ni kuleta hamasa ya mchezo huo katika
jiji la Mbeya.
Aidha katika hatau nyingine Malafyale alibainisha zawadi kwa
washindi ambapo wa kwanza katika ligi hiyo inayo shirikiisha timu 22 kutoka
jiji la Mbeya kuwa bingwa katika michuano hilo ataondoka na kitita cha shilingi
milioni 2,000,000/, wa pili milioni moja wakati huohuo mshindi tatu
atajinyakulia shilingi laki tano.
Naye Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa ligi hiyo kamanda wa
Polisi wilaya wa Mbeya OCD Richard Mchovu aliwataka wachazeji hao kuonyesha nidhamu
katika michezo yote na kwamba sifa ya mchezso kufanya vizuri ni nidhamu.
Aidha alipongeza kwa uamuzi ulifanywa na kampuni hiyo umelisadia
jeshi la Polisi kupiga vita uhalifu kwani muda mwingi ambao wachezaji pa pamoja
na mashabiki wakikuwa vijiniweni ama kupanga mipongo ya kufanya uahalifu
watakuwa viwanjani kwa ajili ya kuingalia michezo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment