HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 16, 2014

KINANA ASHIRIKI FUTARI ILIYOANDALIWA NA MTEMVU DAR

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa na Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu alipowasili, kwenye futari iliyoandaliwa na mbunge huyo Julai 15, 2014, kwenye hoteli ya City Garden, Railyway Gerezani, Dar es Salaam. Pamoja na Kinana ambaye alikuwa mwalikwa rasmi, viongozi na watu kadhaa walihudhuria futari hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiongozana na Mtemvu (kushoto) kuingia ukumbini, kwenye futari hiyo
Mtemvu akimkaribisha kwenye futari hiyo, Mkurugenzi wa Home shpping Centre, Said Gharib. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na kulia ni Mbunge wa Ilala Iddi Azan Zungu.
Kinana (watatu kulia) akipata chai kwanza wakati wa kufuturu futari hiyo
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana (kushoto) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Temeke, Mtemvu wakati wa futari hiyo, Katikati ni aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Haji Manara.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akiendelea kupata chai na wenzake kwenye futru hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge, akifuatiwa na Mtemvu
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana (wapili kushoto) akifuturu na viongozi wengine waalikuwa. Kushoto ni Mbunge wa Temeke, Abbasi Mtemvu na Watatu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabina akifuatiwa na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Juma Kassim.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana (wapili kushoto) akifuturu na viongozi wengine waalikuwa. Kushoto ni Mbunge wa Temeke, Abbasi Mtemvu na Watatu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabina akifuatiwa na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Juma Kassim.
 Sheikh Ali (kushoto) kutoka Ofisi ya Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akishiriki kufuturu futari hiyo huku akiwa meza moja na wadau wengine walioalikwa.
Waalikwa wakijisevia futari
Waaalikwa wakijisevia futari
Kinamama wakipata futari kwenye hafla hiyo ya kufuturisha
Kinana mama wakipata futari
Msanii wa Bongo Movie, Ndugu Mtambalike (kulia) pia alikuwepo, hapa anapata futari na wadau
 Mtemvu akiwashukuru wadau kwa kuhudhuria kwa wingi kwenye futari hiyo, huku akisema kualikana futari si utaratibu mpya bali ni jadi yake ambayo amekuwa akiifanya kwa muda mrefu kila wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kama huu unaoendelea.
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Juma Kaasim akimshukuru Mtemvu kwa kufuturisha na pia kuwashukuru wale wote walioitikia mwaliko wa futru hiyo.
Mtemvu akiongozana na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kutoka ukumbini baada ya futari, Kulia Katibu Mwenezi wa CCM  mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

No comments:

Post a Comment

Pages