HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 15, 2014

MADUKA MATATU YATEKETEA KWA MOTO MWANANYAMALA

 Moto ukiwa umeanza kama utani, watu wakiwa wanaendelea na kazi kama kawaida.
 Moto ukiwa unazidi pamba moto katika duka la kushonea nguo na kuuza vitambaa.
 Duka la nguo likiungua moto na maduka mengine yakiwa yameanza kushika moto.
 Mmoja ya vijana akiwa anaanza kuokoa vitu vyake jirani na maduka yaliyokuwa yakiungua.
 Moto ukiwa unazidi
 Mamia ya watu wakiwa wamefika kushuhudia  tutuki la Moto
 Kazi za uokoaji zikiwa zimeanza huku wasamalia wema wakisaidia kuhamisha vitu
 Maduka mengine yakiwa yameanza kushika moto kwa kasi
 Kazi ya uokoaji ikiwa inaendelea
 Mashuhuda wakiwa wanaongezeka.
Vijana wasamalia wema wakiwa wameacha kazi zao za kutengeneza magari, kufyatua matofari na mambo mengine wakiwa wanafanya kazi ya kuanza kuuzima moto.
 Vijana wakiwa wameanza kufanya kazi ya kuzima moto baada ya Kikosi cha zima moto kuendelea kuchelewa kufika
Maduka yakizidi kwisha kwa kuteketea kwa moto, Huku wananchi wakipata tukio moja kwa moja
 Baadhi ya Vijana wasamalia mwema wakiwa wanaondoa mabati ili kuzuia moto usiendelee kuwaka zaidi

 Watu wakishuhudia.
 Vijana wakiwa bize wakifanya kazi ya kuendelea kuzima moto kwa ushirikiano
 Mmoja wa Mashuhuda akiwa anachukua tukio kwa umakini.
 Kikosi cha zima moto wakiwa wakiwa wanawasili eneo la tukio, huku wananchi wakiwazuia wasifanye kazi kwa kuwa kazi wamekuta imeisha
 Kikosi cha zima moto wakiwa wameanza shuguli ya kumalizia kuzima moto.
 TANESCO wakiwa wamefika eneo la tukio
 Kikosi maalum cha zima moto wakiwa wanamalizia kazi ya kuzima moto kidogo uliobakia.
Kazi ya kuzima moto ikiwa imeisha, mmoja ya wanakikosi cha wazima moto akiwa anafunga mtambo
 Hivi ndivyo maduka yalivyobakia pamoja na nyumba iliyoungua.
 Mmoja wa mashuhuda akiwaelezea jinsi moto ulivyotokea na kushukuru wananchi na Kikosi cha Zima Moto kwa kazi kubwa iliyofanikisha zoezi ka kuzima moto.


*******
Moto mkubwa uliosababishwa na hitirafu ya umeme  umewaka eneo la Mwananyamala jirani na Hospitali ya Mwananyamala na kusababisha kuungua kwa Maduka matatu pamoja na nyumba moja ambayo ilikuwa imeungana na duka moja wapo ambamo walikuwa wanauza vitambaa na kushona nguo.

Moto huo ulichukua zaidi ya masaa mawili ambapo wakazi wa eneo hilo ndio waliosaidia kwa kiasi kikubwa kuzima moto huo mpaka kuumaliza na baadae Kikosi cha kuzima moto kufika na kukuta moto ndio unaishia na kuendelea kumalizia kushirikiana na wananchi wengine kuzima moto huo.

Katika tukio la Moto huo hakuna mtu ambaye amedhuriwa ingawa katima maduka yote matatu walifanikiwa kuokoa baadhi ya vitu huku vilivyobakia kuteketea vibaya kwa moto huo. Picha zote na Dar es salaam yetu Blog

No comments:

Post a Comment

Pages