Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na
mkewe mama Salma Kikwete wakiangalia mandhari ya mji wa Pangani wakati wa ziara
ya kikazi wilayani humo.Sehemu kubwa ya mji huo imo katika hatari ya kumezwa na
bahari kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na serikali imeahidi kujenga ukuta
pembezoni mwa mto Pangani ili kuzuia athari za kimazingira kutokana na
kuongezeka kwa kina cha maji.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipitia moja ya hotuba zake akiwa ndani ya kivuko
kipya cha MV Pangani II wakati akivuka mto Pangani kutoka Tarafa ya Bweni
kuelekea Pangani mjini wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Pangani. Rais Kikwete ambaye alikuwa mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi ya
wiki moja alihitimisha ziara hiyo jana ambapo pamoja na mambo mengine alisema
kuwa serikali itajenga kivuko kingine kwenye mto huo chenye uwezo mkubwa zaidi
ili kuboresha shughuli za kiuchumi na kijamii wilayani humo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya majumuisho wakati akihitisha
ziara yake ya kikazi ya wiki moja mkoani Tanga ambapo alizindua na kukagua
shughuli mbalimbali za maendeleo(picha na Freddy Maro)
No comments:
Post a Comment