Taasisi hewa za fedha zinazodai kutoa mikopo kwa njia ya simu za mikononi.
Napenda kuwafahamisha wananchi kujihadhari na utapeli unaofanywa na baadhi ya taasisi hewa hapa nchini zinazodai kutoa mikopo kwa wananchi kwa njia ya simu za mikononi.
Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwepo na ongezeko la Taasisi hewa za fedha zinazotoa huduma kwa njia ya mitandao ya simu za mikononi na kuwaadaa wananchi kwa kutumia majina ya viongozi wa serikali, viongozi wa siasa na taasisi kubwa za kibenki.
Taasisi hizo pia uweka namba za uongo za usajili kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwagilibu wananchi kuwa taasisi hizo ni halali.
Mathalan, taasisi inayojiita Social credit Loans inayoeleza kuwa imesajiliwa TRA kwa namba Reg. No.33/SCC/REG/REG/7894 na namba ya utambulisho ya mlipa kodi TIN: 203-344-6789.
Ufuatiliaji uliofanywa na TRA umebaini kuwa hakuna taarifa zozote kuhusu taasisi hiyo.
Taasisi nyingine ni Saving Foundation na Quicken Loan.
Utendaji wa taasisi hizi hutegemea mitandao ya simu za mikononi, mfano;
-Kupokea fedha za waliojaza fomu zinazopatikana katika tovuti zao, na-Kutuma mikopo.
Nambari wanazotumia ni 0715 373 307, 0755 066 858, 0752 567 717 na 0654 441 494.
Pia napenda kuwakumbusha wananchi wote kwa ujumla wakiwemo watumishi wa umma kutokubali maombi ya fedha, fadhila au maelekezo yanayodaiwa kutolewa na uongozi wa juu bila kupata uthibitisho kutoka mamlaka husika.
No comments:
Post a Comment