HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

July 07, 2014

WASHINDI WA DROO YA MeTL GROUP WAPATIKANA KATIKA MAONYESHO YA SABASABA

 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (wa pili kulia) akimtangaza mshindi wa droo maalum kwa wateja wanaotembelea banda la MeTL GROUP kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea  katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere,  barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.Na Mshindi huyo ameshinda Zawadi ya Pikipiki aina ya A1 ambayo imesajiliwa na seti mbili ya Vitenge,Wa kwanza kushoto ni msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Bahatinasibu Bwana Mrisho Millao.Wanaoshuhudia wa pili kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL Group, Kelvin Msangi na Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali (wa Kwanza kulia).
Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bw. Mrisho Millao akichanga boksi lenye majina ya wateja waliotembelea Banda la kampuni ya MeTL GROUP na kujaza kuponi za kushiriki kwenye droo ya Bahati nasibu kwenye Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea  katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere,  barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.Mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa (wa pili kulia), Meneja Masoko wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali (kulia) na Msaidizi wa Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya MeTL Group, Kelvin Msangi (wa pili kushoto) wakishuhudia tukiao hilo.

No comments:

Post a Comment

Pages