HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

July 07, 2014

BENKI YA CRDB YAWASHAURI WAZAZI KUWAFUNGULIA WATOTO AKAUNTI YA JUMBO JUNIOR

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB imewataka wazazi kuwafungulia watoto akaunti ya Junior Jumbo kwa ajili ya akiba yao ya baadae.

Akizungumza katika maonesho ya 38 ya biashara ya Kimataifa Dar es salaam, Ofisa Masoko wa CRDB, Nazareth Kipingo, alisema akaunti hiyo ni kwa ajili ya watoto ambapo mzazi huifadhi fedha kwa ajili ya ada au akiba ya mtoto  katika maisha yake ya baadae.

Alisema akaunti hiyo itamsaidia mzazi kuweka fedha kimkakati ambapo atatakiwa kutoa mara nne kwa mwaka katika msimu wa ada ya shule na kuongeza kuwa CRDB pia inaweza kumlipia mtoto  ada kwa utaratibu maalum.

Kipingo alisema Jumbo junior ni akaunti inayomhakikishia mtoto  elimu ya uhakika na kupunguza kero za kulipa ada kwa mkupuo kutoka mfukoni mwa mzazi.

Alisema kuwa katika maonesho hayo wanaendesha huduma za kibenki katika viwanja hivyo ili kumpunguzia mteja adha ya kutembea na pesa.
Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Julius Ritte akiwahudumia wateja wapya waliofika katika Banda la CRDB kupata huduma za kibenki. 
 Mteja wa Benki ya CRDB akijaza fomu kwa ajili ya kufungua akaunti.
 Watu mbalimbali walifurika katika Banda la Benki ya CRDB kwa ajili ya kufungua akaunti mpya pamoja na kupata huduma mbalimbali za kibenki zinazotolewa na Benki ya CRDB.
Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma za kibenki kutoka katika tawi linalotembea (Mobile Branch), wakati wa Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages