HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 16, 2014

MBILE V/S MSHALE DIMBANI KESHO, MSHIKAMANO CUP

NA SILVESTER DAVID

TIMU za soka za Mbile FC na Mshale FC leo zitashuka dimbani katika mechi ya fainali ya kuwania ubingwa wa michuano ya Kombe la Mshikamano itakayopigwa uwanja wa Kinnes, Urafiki, jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia mechi hiyo,  Rama Risasi ‘No Fear’ ambaye ni kocha wa Mshale FC, alisema mechi hiyo itakuwa ngumu kutokana na kila moja kukamia ushindi kutwaa ubingwa.

Alisema kama vijana wake watacheza vizuri kama mechi zilizopita tangu kuanza kwa michuano hiyo Juni 29 katika hana hofu na ubingwa.
Alisema michuano hiyo iliyoshirikisha jumla ya timu 10, mechi za robo fainali zilipigwa katika viwanja vya Las Vegas, Mabibo na kuanzia nusu fainali zikahamia Uwanja wa Engo, Kinesi Urafiki.

“Kesho (leo) sisi Mshale FC tutacheza mechi ya fainali dhidi Mbile FC, nawasihi wapenzi na mashabiki wetu waje kutushangilia, tumejipanga vizuri kuibuka mabingwa,” alisema Risasi.

Alisema kwa upande wao wamejiandaa vizuri kwani vijana wake wamekuwa wakicheza soka ya uhakika tangu kuanza kwa michuano hiyo ambapo hadi kufikia fainali ya leo, timu yake haijapoteza mechi. 

Kuhusu zawadi, Risasi alisema bingwa atapata Kombe na jozi 30 za jezi; mshindi wa pili ataondoka na mbuzi huku kukiwa hakuna zawadi kwa mshindi wa tatu.

Aliongeza kuwa, lengo la michuano hiyo ni kuibua na kukuza vipaji vya vijana, kukuza umoja miongoni mwa wachezaji, kuboresha afya na kuamsha ari ya vijana kupenda michezo. Risasi alisema mgeni rasmi katika mechi ya leo, atakuwa ni
Seleman Masawe.

Akielezea  upande wa timu yake ya Mshale alisema,wamejipanga vizuri kwa ajili ya kuchukua kikombe hicho kwani wachezaji wote wako vizuri kiafya hivyo mashabiki wategemee soka safi kutoka kwenye timu yake lakini haibezi timu pinzani na kueleza kuwa mpira ni dakika 90.

No comments:

Post a Comment

Pages