HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 19, 2014

MILEMBE INSURANCE KUNOGESHA TAMASHA LA KWANZA LA MAGARI LA ‘AUTOMOBILE CLINIC’ JIJINI DAR

Mmiliki wa Jossekazi Auto garage ambao ndiyo waandaaji wa tamasha akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la kwanza la Magari la aina yake, linalojulikana kwa jina la Automobile Clinic, ambalo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili Septemba 27 na 28, 2014 katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam. Ambapo alisema kuwa tamasha hilo limelenga katika kutoa huduma ya kitaalamu ya kiufundi kwa wenye magari (Checkup and Fix) kutoka kwa mafundi stadi ambao wamebobea katika fani ya ufundi wa makenika katika aina tofauti tofauti za magari. Pembeni kulia ni Mkurugenzi wa Jast Tanzania Limited, Jahu Mohammed Kessy, Mratibu wa Tamasha hilo na Mwakilishi toka Mwambi Lube Distributor, Jonathan Mwanayongo.

Na Mwandishi Wetu. Kampuni ya Jast Tanzania Limited kwa kushirikiana na Jossekazi Auto Garage and General supplier wameandaa tamasha la kwanza la Magari la aina yake, linalojulikana kwa jina la Automobile Clinic, ambalo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili mfululizo katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam. Tamasha hilo limelenga katika kutoa huduma ya kitaalamu ya kiufundi kwa wenye magari (Checkup and Fix) kutoka kwa mafundi stadi ambao wamebobea katika fani ya ufundi wa makenika katika aina tofauti tofauti za magari.

Akizungumza na vyombo vya habari, kwenye ukumbi wa habari Maelezo, Joseph Mgaya mmiliki wa Jossekazi Auto garage amesema tamasha hili lina lengo kuwakutanisha mafundi stadi na wenye magari, kwa gharama nafuu sana ya shillingi elfu ishirini tu.
Mkurugenzi wa Jast Tanzania Limited, Jahu Mohammed Kessy, Mratibu wa Tamasha hilo akielezea machache juu ya tamasha hilo.
Mgaya alisema huduma hizo ambazo zilipaswa kugharimu kiasi kikubwa sana cha pesa kwa wenye magari, kitatolewa kwa bei nafuu ili kwa makusudi tu ya kukutanisha mafundi hao na wenye magari.

Alisema pamoja na Wateja kutengenezewa Air condition na kujaziwa gesi, kufanyiwa Electronical scan diagnosis, Kuchekiwa Matairi, kuchekiwa Battery, na kupata ushauri wa kiufundi kuhusu gari zao, pia tamasha hilo litakuwa ni sehemu ya kukutanisha watu na kupata burudani.

Mgaya alisema, Mafundi wapatao 50 waliobobea katika fani ya ufundi magari, wamepatikana baada ya kufanyiwa usaili wa kina na kupitia mchujo na semina elekezi ili kuweza kuhudumia magari yanayokadiriwa kufika zaidi ya 6000 kwa siku hizo mbili.

Pamoja na hayo, Mgaya alisema “ Tumeandaa warsha maalum kwa kina dada, tunatambua kuwa asilimia kubwa ya waendesha magari barabarani hivi sasa ni kina dada, tunataka waelewe ni nini cha kufanya pindi atakapopatwa na hitilafu kwenye gari mabarabarani. “

Elimu hii ambayo wameiita ‘Auto First Aid’, alisema itasaidia kupunguza uharibifu zaidi kwenye magari yao, alisema wakati mwingine kwenye dashboard ya gari kuna kuwa na alama za hatari, lakini kwa kuwa gari inatembea wanawake wengi wamekua wakipuuzia alama hizo na matokeo yake wanasababisha hasara kubwa zaidi.
Afisa Mkuu wa Fedha wa Milembe Insurance, Dioniz Diocles (wa kwanza kulia) akiongea mbele ya waandishi wa habari kuelezea jinsi walivyoona umuhimu wa kudhamini tamasha hilo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Jast Tanzania Limited, Jahu Mohammed Kessy, Mratibu wa Tamasha hilo, Mmiliki wa Jossekazi Auto garage ambao ndiyo waandaaji wa tamasha, Mwakilishi toka Mwambi Lube Distributor, Jonathan Mwanayongo. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

No comments:

Post a Comment

Pages