NSSF kupitia mpango wake wa Wakulima Scheme yadhamini mechi ya kujipima nguvu kati ya Simba ya Dar es Salaam na Ndanda FC ya Mtwara kwenye uwanja wa CCM wa Nangwanda Sijaona na kuhudhuriwa na maelfu ya washabiki wa soka mkoani Mtwara.
Mchezo huo pia ulikuwa ni sehemu ya sherehe za Ndanda Day ulihudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo wa Serikali uliisha kwa matokeo ya timu hizo kutoka suluhu.
NSSF kupitia mpango maalum wa wakulima schemes wenye lengo la kuandikisha na kuhudumia wakulima kwenye mfuko ya hifadhi ya jamii nchini ili kuwawezesha wakulima wote nchini wawe kwenye mfuko wa huo kupata pensheni ya uzeeni pindi watakapo fikisha umri wa miaka 55 na kuendelea wakulima hao wataweza kulipwa penshion zao hadi watakapo fariki.
Mpangu huu unamwezesha mkulima kupitia chama cha wakulima AMCOS kuweza kupata mkopo na taarifa muhimu kuhusu wakulima,wakulima wanachama wa NSSF wanajiunga bure na kuchangia kuazia shilingi 20,000 na kuendelea.
Aidha mpangu huu unampa mkulima nafasi pekee ya kulipa kwa msimu wa mavuno yaani msimu wa mavuno anaweza kulipia kwa mwaka mzima, miezi anayoweza lipia, lakini pia wakulima wanaweza lipia baada miezi iliyopitilizia bila malipo msimu wa mavuno.
NSSF likiwa ni shirika pekee lenye kuwapa huduma ya afya bure wanachama na kuwawezesha wanachama kutoyumba kiuchumi kwa sababu za gharama za matibabu kwenye familia.
NSSF linawahudumia familia ya mwanachama kwa kuwapa matibabu bure watoto wanne mwanachama na mwenza.matibabu haya wanapata pia wakulima wanaojiandikisha kwenye mpango huu wa SHIB wa NSSF na kuwawezesha kuokoa vipato vyao ambavyo vingetumia kwenye matibabu.
NSSF mkoa wa mtwara unampango wa kuandikisha wanachama 63,000 kutoka kwa wakulima wa vijiji na wilaya zote mkoani mtwara ambazo ni Tandahimba,Nanyumbu,Masasi ,Nachingwea,Newala,Mtwara Vijijini ambao wengi ni wakulima wa zao korosho.
Pia kwa akina mama wanapata mafao ya uzazi,kabla na baada ya kujifungua.aidha wakuliwa wataweza kupata mikopo kupitia SACCOS zao na kuwawezesha kununua mbolea,madawa ya kuulia wadudu,pembejeo,dhana mbali mbali za kilimo ili kujiinia kiuchumi kupitia NSSF SACCOS Loans.
Ofisi ya NSSF Mkoa wa Mtwara umeshatoa jumla ya shilingi Bilion 1.75 kwa SACCOS zilizokidhi vigezo na kuwainua kimaisha wajasiriamali, wakulima na wafanyakazi.
Wachezaji wa Simba na Ndanda FC wakiingia Uwanjani wakati wa
mchezo wa maalum wa kusherehekea Ndanda Day uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na kudhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
kupitia mpango wake wa Wakulima Scheme. Timu hizo zilitoka suluhu. (Na Mpiga
Picha Wetu)
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu Joseph Simbakalia akisalimia na timu ya Ndanda FC kabla ya mchezo wao na timu ya Simba uliofanyika leo kwenye Uwanja wa
Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu Joseph Simbakalia akikagua timu ya Simba wakati wa mchezo wa kirafiki na timu ya Ndanda FC uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Kikosi kamili cha timu ya Simba kilichopambana na Ndanda FC.
Kikosi cha Ndanda FC kikiwa klatika picha ya pamoja kabla ya pambano lao na Simba.
Kikosi cha Ndanda FC kikiwa klatika picha ya pamoja kabla ya pambano lao na Simba.
Wachezazaji wa Simba na Ndanda wakichuana katika uwanja wa Nangwanda Sijaona.
No comments:
Post a Comment