HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

September 23, 2014

SHAMSA FORD SASA KUCHEZA FILAMU ZA KIUHALISIA

NA ELIZABETH JOHN

MWANADADA anayetamba katika tasnia ya filamu nchini, Shamsa Ford, amesema ameamua kuanza kufanya filamu zinazogusa maisha ya watu ili kuleta maana kwa wale watazamaji na siyo stori za kubuni. 

Akizungumza jijini Dar es salam juzi, Shamsa alisema kuwa amecheza filamu nyingi sana za stori zisizo kuwa na uhalisia japokuwa zilikuwa zinasisimua mashabiki. 

“Ni vyema sasa kufanya filamu zinazogusa maisha yanayotuzunguka kwa sasa ili mtazamaji aweze kuelewa nini kinaendelea kwa jamii inayomzunguka,” alisema. 

Shamsa aliongeza kuwa, hali imekuwa mbaya kiuchumi, kiakili na hata kifikra, hivyo wao kama wasanii wanapaswa kucheza filamu za maisha halisi ili wanaozitazama wapate vitu muhimu vya kujirekebisha. 

“Tumezungukwa na maisha ya watu ambayo kila unapowaangalia baadhi yao roho inauma na kushindwa uanzie wapi kuwasaidia, hivyo sina budi kucheza muvi inayoendana na maisha yanayotuzunguka. Huo utakuwa msaada tosha kwa wanaotazama na kujua tunaanzia wapi kusaidiana,” alisisitiza Shamsa. 

Alisema kuwa, kwa sasa amekuja kitofauti zaidi kwani Shamsa aliyekuwa anacheza filamu zamani, siyo wa sasa ana mambo mengi ambayo wadau watayaona katika filamu inayoendelea kuwika nchini iitwayo ‘Chausiku’.


No comments:

Post a Comment

Pages