Na Mwandishi Wetu
ASKOFU wa Kanisa la
Hossana Life Mission Ephraim Mwansasu, amewataka Watanzania kutowachagua
wanasiasa ambao wako tayari kumwaga damu ili mradi wapate madaraka katika
uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza na wandishi
wa habari wakati wa ibada ya kuliombea Taifa, iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Askofu Mwansasu, alisema kuna ishara ambazo zinaashiria kuvurugika amani.
Alisema ili kuepuka
kuvurugika kwa amani na kumwaga damu nchini ni vema Watanzania wakajiandaa
kuchagua viongozi ambao hawako tayari kuona damu ina mwagika.
“Mwanasiasa yeyote
anayenuia mabaya tusimkubali hata itikadi anayosema madhali anakusudia mabaya
tunaenda kuwashusha kwa jina la bwana,”alisema Askofu Mwansasu.
Askofu, alisema wako
tayari kumuombea kiongozi yeyote, ambaye anaonesha nia ya kudumisha amani,
umoja na kupigania haki za wanyonge, ili awezekuchaguliwa hata kama hana uwezo
wa kifedha.
Akizungumzia ishara
nyingine ambazo zinaweza kuliingiza taifa katika mifarakano ni vitendo vya
polisi kuingia kwnye migogoro na
wandishi wa habari.
Askofu Mwansasu,
alisema kitendo cha kupigwa wandishi wahabari ni jambo la hatari ambalo
linaweza kuliingiza taifa katika machafuko yasiyotarajiwa.
“Ufike wakati vyombo
hivi muhimu ambavyo vinategemeana sana katika majukumu yao ya kila siku, hivyo
ni vema vikaheshimiana ili kila kimoja kijiamini kwa mwenzake”alisema Askofu
Mwansasu.
Aliongeza kwa kusema
kuwa hata matabaka yanayojitokeza katika vyama vya siasa vikiwemo vikubwa na
vidogo, nayo pia yanatishia kuvurugika kwa amani, yote hayo yanapaswa kuombewa
ili vyama hivyo viweze kuwa na mshikamano kwa ajili ya kuzalisha viongozi bora.
No comments:
Post a Comment