Na Ibrahim Yassin, Rungwe
IMEELEZWA kuwa wananchi wa kata ya Mpuguso iliyopo wilayani
Rungwe mkoani Mbeya wamekuwa wakitembea umbali
wa kilometa kumi na tano kufuata huduma ya afya kutokana na kata hiyo
kutokuwa na kituo cha afya wala zahanati tangu nchi ya Tanzania ipate uhuru
1961.
Kauli hiyo ilitolewa na diwani wa kata ya Mpuguso
wilayani humo,Tibandelage Kalinga kwenye kikao cha kawaida cha baraza la
madiwani am,bapo aliiomba Halmashauri ya wilaya hiyo kuwa ni lini itajenga
kituo cha afya na zahanati katika kata yake.
Tibandelage ambaye ni diwani wa kata hiyo kupitia Chadema
alilieleza baraza hilo kuwa wananchi wake wamekuwa wakipata na kadhia hiyo
ambapo akina mama wajawazito na watoto baadhi yao wamekuwa wakipoteza maisha
kabla hata hawajafika hospitalini kutokana na umbali mrefu.
Alisema katika kata hiyo kuna viwanja vya wazi vingi na kutoa
yeye kutoa maombi kwenye halmashauri hiyo kuhitaji kujengewa zahanati na kituo
cha afya lakini amekuwa akiwekewa ngumu kutokana na kata hiyo kuongozwa na
kambi ya upinzani katika ngazi ya kijiji hadi kata.
Alisema kutosikilizwa kwa tatizo hilo hasa mateso wanayopata
wananchi wa kata hiyo ya kutembea umbali mrefu kumetokana na itikadi za kisiasa
kwa kuwa kata hiyo inaongozwa na kambi ya upinzani na kwamba wanakwamisha
jitihada hizo ili wananchi waone kama wao hawafanyi kazi.
Akijibu hoja hizo mkuu wa wilaya hiyo Chrispin Meela alisema
kata hiyo ilikuwa na uwanja ambao ulitakiwa ujengwe zahanati lakini
ilishindikana kutokana na kuwa uwanja huo unamatatizo kati ya mtu na kijiji
hadi kufikia hatua ya kupelekana mahakamani na kukwamisha jitihada hizo.
Alisema suala la ujenzi wa miradi linaanzishwa na wananchi
wenyewe kazi ya serikali ni kuunga mkono nguvu kazi hizo kwa kusaidia kupaua na
si kuanzisha kujenga na kuwa wananchi na viongozi wa kata hiyo wanatakiwa
kutafuta uwanja mungine na kuanzisha ujenzi kisha serikali itasaidia kupaua.
No comments:
Post a Comment