Na Ibrahim Yassin, Rungwe
MTUMISHI wa Halmashauri Idara ya Maendeleo ya Jamii Wilayani
Rungwe mkoani Mbeya Benjamini Kaswaga (50) amekutwa amekufa chumbanii kwake
tarehe 16/10/2014 aligundulika na majirani majira ya saa mbili usiku
baada ya kuona hakutoka nje ya nyumba yake tangu alipoingia.
Akizungumzia tukio hilo kwenye kikao cha Baraza la madiwani
kilicho keti jana mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Vironica Kessy alisema katika
uhai wake Benjamini alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kuanguka na kwamba kifo
chake uenda kimetokana na tatizo hilo.
Alisema kuwa mtumishi huyo hakuwa na mke hivyo kutoonekana
kwa siku mbili huku mlango wa nyumba yake ukiwa umefungwa ndipo majirani
walianza kuwa na shaka ambapo walipo sogea walisikia harufu mbaya ikitoka katika
nyumba hoyo na kuamua kutoa taarifa polisi.
Aliongeza kuwa jeshi polisi wilayani humo lilifika eneo la
tukio na kuamuru kuvunja mlango mbele ya wananchin wakiwa na viongozi wa kijiji
ambapo wakuta mtumishi huyo amekufa na kwamba baadaye mwili huo ulipelekwa hadi
kwenye hospital ya wilaya kwa uchunguzi.
Mganga mkuu wa wilaya Ndagabwene Sungwa alisema tatizo la kifo cha mtumishi huyo hawezi kulitolea maelezo.
Madiwani na watendaji katika halmashauri hiyo wameambatana na
familia hiyo kwenda katika maandalizi ya mazishi ya mtumishi huyo
yatakayofanyika kesho wilayani humo na kusema kuwa
walimpenda lakini mungu alimpenda zaidi,
No comments:
Post a Comment