JUMUIYA ya
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini (Tahliso), imeshangazwa na kauli ya Mkurugenzi
wa Elimu ya Juu Profesa Sylivia Temu, kwamba wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi haiwezi kutekeleza madai ya wanafunzi hao hadi itakapopata barua rasmi.
Kauli ya
Profesa huyo inakuja siku chache baada ya taarifa ya hivi karibuni iliyotolewa
na Tahliso kupitia vyombo vya habari kuhusu maombi yao ya kuongezewa fedha za
kujikimu kutoka sh 7,500 hadi sh 15,000 kwa siku kutokana na madai ya kupanda
kwa gharama za maisha.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Rais wa Tahliso, Mussa Mdede,
alisema anamini wizara inazo taarifa rasmi ikiwemo ile ya kuwapatia wanafunzi
wote 58037 waliomba mkopo.
Alisema
kauli ya Profesa huyo haina ukweli kutokana na jumuiya hiyo ikiwa katika
mkutano mkuu mkoani Iringa, Setemba 26 mwaka huu, ilituma Fax ya maazimio ya
mkutano huo kwa waziri wa wizara hiyo na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Aliyataja
baadhi ya maazimio hayo kuwa ni masuala ya vyuo kuwapandishia wanafunzi ada
kiholela vikikiuka maagizo ya TCU.
“Tunapinga
kauli ya Bodi ya Mikopo kutoa mkopo kwa wanafunzi 30,000 huku wengine 28,037
wakikosa, sasa maazimio yetu tuliyoazimia tunataka wote wapate mikopo bila
kubaguliwa.
“Kwa kuwa
niko safarini mkoani Mwanza, nimemuagiza katibu mkuu wa Tahliso kuwa
anahakikishe kabla jua halijazama leo kwamba anaifikisha barua hiyo
wizarani,”alisema kwa njia ya simu.
Mdede,
alisema licha ya mambo yote hao, bado dhamira yao nikukutana na waziri wa
wizara hiyo ili kuzungumzia mustakabali wa elimu ya juu nchini.
No comments:
Post a Comment