Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. DK. Mary Nagu ametembelea
Kiwanda cha kutengeneza unga cha Basic Element ltd jana Novemba 10, 2014 Dar es
Salaam. Waziri Nagu alitembelea sehemu za kiwanda hicho ili kuona teknolojia
wanayotumia kiwandani hapo, nafaka zilizopo na namna wanavyoweka unga tayari
kuuza. Katika zoezi hilo aliwapongeza na kuwataka Watanzania kutumia fursa hiyo
kwa kununua unga unaotengenezwa na kuwahakikishia wakulima kutasaidia kupata
soko la kuuza mazao yao.
Mhe.
Nangu alitoa wito kwa watanzania kuunga mkono kazi zinazofanyika nchini kwa
kununua unga unaopatikana ikiwa ni salama na wenye ubora unaofaa kwa mlaji. Pamoja
na hilo Waziri Nagu alisema, uwepo wa kiwanda hicho ni sehemu ya vijana
kujipatia ajira kwani wanatoa nafasi 50 za ajira.
Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu
Kitengo cha Mawasiliano
Tarehe 11 Novemba, 2014.
Mhe. Mary Nagu akipata maelezo akiangalia bidhaa zinazozalishwa na Kiwanda cha
kutengeneza Unga cha Basic Element Ltd Dar es Salaam.
Mhe. Mary Nagu akipata maelezo alipotembelea Kiwanda cha
kutengeneza Unga cha Basic Element Ltd Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment