NA KENNETH NGELESI, MBEYA
KAMPUNI inayo jihusisha uzalishaji wa Vinywaji baridi nchini (Pepsi)
SBC Limited Mkoa wa Mbeya imetangaza shindano la jishindie mamilioni kila siku na Peps kwa wakazi wa mkoa huo kwa lengo la
kuwawezesha wananchi kujikomboa na hali ya kiuchumi.
Akizungumzia shindano hilo jana,Meneja
mkuu wa SBC,Sanjay Munshi alisema kampuni hiyo imetangaza shindano hilo kwa
lengo la kuwawezesha wananchi kujipatia zawadi mbalimbali zikiwemo soda na
fedha taslimu kwenye soda.
Aidha Meneja huyo alibanisha soda
ambazo zinazalihswa na kiwandoa hicho ambazo zitakuwa na zawadi kuwa za Pepsi,Mirinda Orange,Mirinda Green Apple,Mirinda
Fruity,Mountain Dew (300ml) na Seven Up zenye ujazo wa 350mil.
Katika hatua nyingine Munishi
alisema kuwa katika shindano hilo,wateja wataweza kujishindia kiasi cha sh
1,000,5,000,10,000 ambazo zitatolewa papo hapo mara baada ya mteja kupata
zawadi hiyo.
Alisema kuwa na kuwa kiasi cha sh.500,000,1,000,000 na
milioni 2,500,000 zitatolewa kwenye ofizi za kampuni hiyo katika mikoa ya Dar
es salaam,Morogoro,Lindi,Mbeya na Iringa katika muda wa kazi kuanzia saa 4
asubuhi hadi saa 9 alasiri.
Munishi alisema kuwa katika shindalo hilo ambalo litafiki tamati
Jenuari 30 mwakami, kila siku kutakuwa na mshindi mmoja wa sh 1,000,000/ huku akiweka wazi kuwa soda zenye bahati nasimu ni
zile zenye vizibo vyenye rangi la dhahabu.
Katika hataua nyingine Meneja huyo alisewma
kuwa shindano hilo litahusisha mikoa 13 amabayo ni Dar essalaam,Mbeya,Morogoro,Pwani, Dodoma,Tanga,Lindi,Mtwara, Iringa
Njombe,Rukwa,Ruvuma na Katavi
Naye Meneja Mauzo wa kampuni Mkoa wa
Mbeya Omari Jumbe, alisema katika shindano la bahati nasibu la kampuni hiyo ya
SBC kwa mwaka jana jumla ya washindi 50 walijishindia zawadi mbalimbali na kuwa
mwaka huu zawadi hizo zimeongezwa mara dufu kwa wateja.
No comments:
Post a Comment