Kikosi cha wachezaji 23 wa Taifa Stars tayari
kimewasili Johannesburg, Afrika Kusini tayari kwa maandalizi ya mechi dhidi ya
Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Swaziland.
Mechi hiyo itafanyika Jumapili (Novemba
16 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa wa Somhlolo jijini Swaziland. Taifa Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwepo Johannesburg hadi Ijumaa
itakapoondoka kwenda Mbabane.
Wachezaji wote walioitwa na Kocha Mart
Nooij wapo kwenye msafara huo isipokuwa kiungo mshambuliaji Mrisho Ngasa ambaye
amebaki Dar es Salaam kutokana na matatizo ya kifamilia.
Taifa Stars inatarajia kurejea nyumbani
Jumatatu (Novemba 17 mwaka huu) saa 12.45 jioni kwa ndege ya South Africa
Airways.
Wakati huo huo, kikosi cha
maboresho cha Taifa Stars kitacheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya
Rwanda kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 23. Mechi hiyo itachezwa Desemba
9 mwaka huu nchini Tanzania.
Kikosi cha maboresho cha Taifa Stars
kinachoundwa na wachezaji wenye umri chini ya miaka 23 kitakuwa kinakutana mara
moja kila mwezi hadi Mei mwakani kwa ajili ya mazoezi na kucheza mechi moja ya
kirafiki.
Kocha Mart Nooij atatangaza kikosi kwa
ajili ya mechi hiyo na programu nzima mara atakaporejea kutoka Swaziland.
WAAMUZI 23 KUSHIRIKI SEMINA DAR
Waamuzi 23 wa daraja la kwanza wakiwemo
wenye beji la Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) wameteuliwa
kushiriki semina itakayofanyika Novemba 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa semina hiyo ambayo pia
itakuwa na mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) wanatakiwa
kuripoti Novemba 15 mwaka huu kwenye hosteli ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) iliyopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Wakufunzi wa semina hiyo wanaotambuliwa
na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni Riziki Majala na Soud Abdi.
Waamuzi watakaoshiriki semina hiyo ni Ahmed
Juma Simba (Kagera), Arnold Bugado (Singida), Charles Peter Simon (Dodoma), Dalila
Jafari Mtwana (Zanzibar), Ferdinand Chacha Baringenge (Mwanza), Florentina
Zabron (Dodoma) na Frank John Komba (Pwani).
Grace Wamara (Kagera), Hellen Joseph
Mduma (Dar es Salaam), Israel Mujuni Nkongo (Dar es Salaam), Issa Bilali Ali
(Zanzibar), Issa Haji Vuai (Zanzibar), John Longido Kanyenye (Mbeya), Jonesia
Rukyaa Kabakama (Kagera) na Josephat Deu Bulali (Tanga).
Kudra Omary (Tanga), Martin Eliphas
Saanya (Morogoro), Mary Kapinga (Ruvuma), Mfaume Ali Nassoro (Zanzibar), Mgaza
Ali Kinduli (Zanzibar), Samwel Hudson Mpenzu (Arusha), Soud Iddi Lila (Dar es
Salaam) na Waziri Sheha Waziri (Zanzibar).
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment