Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, akikata
utepe kama ishara ya kukabidhi vibanda vya kisasa vya Airtel Money kwa watu
wenye ulemavu, wanachama wa Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo Watu wenye
Ulemavu (HREDP). Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kulia kwake
ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano na kulia ni Mwenyekiti
wa taasisi hiyo, Abubakar Rakesh na mnufaika wa kibanda hicho, Hebron Mwansele
(mwenye baiskeli). (Na Mpiga Picha Wetu)
Kuwapatia vioski vya biashara na mtaji kuanzisha biashara
·
Kuwawezesha kujiinua na kuwa wajasiriamali
Katika kuendeleza shughuli
zake za huduma kwa jamii kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imekabidhi
vibanda vya kisasa vya Airtel Money kwa watu wenye ulemavu yenye lengo la
kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wajasiriamali.
Sambambal na hilo Airtel pia
imewapatia mtaji wa kuanzisha biashara ili kuwawezesha watakao nufaika na
vibanda hivyo kuwa mawakala wa huduma ya Airtel money na kutoa huduma
mbalimbali ikiwemo kuuza bidhaa za Airtel kupitia vibanda hivyo vilivyo katika
sehemu mbalimbali jijini Dar es Saalam.
Akiongea wakati wa hafla ya
makabidhiano , Naibu Waziri wa mawasiliano Mh. Januari Makamba alisema”
tunapenda kuwashukuru Airtel kwa kutanua wigo na kutoa msaada kwa watu
wenye ulemavu ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi. Serikali yetu iko
makini katika kuhakikisha kila mtanzania anapata haki sawa bila kubagua makundi
natoa fulsa sawa katika maeneo mbalimbali.
Sisi kama Serikali tunaamini
msaada mliopokea leo utakuwa chachu ya kuleta maendeleo ya kiuchumi na nyenzo
kwa wanachama wa Taasisi ya haki za binadamu na maendeleo ya kiuchumi kwa watu
wenye ulemavu kujikwamu na tatizo la kiuchumi unaowakumba makundi mengi kama
haya katika jamii”.
Sera ya serikali kwa
walemavu inalenga kuboreshea mazingira watu wenye ulemavu na kuwahusisha katika
shughuli za uzalishaji ili kuinua uchumi na kutumia kwa ufanisi rasilimali
zilizopo katika kuboresha huduma. Naaamini kwa Airtel kuwekeza kwenye jamii leo
hakutachangia kuboresha maisha ya wengi tu bali kutachangia kutekeleza na
kutilia mkazo agenda za Serikali.
Nachukua fulsa hii kuwaomba
makampuni mengine na wadau mbalimbali kushirikiana na serikali katika kutoa
misaada ya muda mrefu na endelevu katika makundi mengine kama haya nchini kama
ilivyofanywa na Airtel leo”. Aliongeza Makamba
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Airtel Bibi Beatrice Singano alisema “ kwa mara nyingine tena
tumefikia jamii kupitia mpango wetu wa huduma kwa jamii tukiamini kwa kufanya
hivi tunachangia na kusaidi familia za wanachama wa Taasisi ya haki za binadamu
na maendeleo ya kiuchumi kwa watu wenye ulemavu , pamoja na kuinua uchumi kwa
watu wenye ulemavu kwa ujumla. Airtel tunatoa fulsa na kuwawezesha wale
waliokuwa na ndoto za kumiliki biashara zao kuweza kuzifikia ndoto hizo na
kujikita kwenye ujasiriamali na biashara.
Tunaamini Msaada huu
haujalenga kuwapatia mtaji tu bali vifaa vya kuendesha biashara pamoja na
mafunzo ya jinsi ya kuendesha biashara endelevu. Tunauhakika ushirikiano
tulioanzisha leo utawaweza wanachama wa kikundi hiki kuwa sehemu ya kutoa
huduma zetu na hivyo kupata faida itakayowawezesha kuwa wajasiriamali bora
nchini’
Tunawaasa wale wote
watakaofaidika na msaada huu leo kutumia vibanda hivi kwa ubunifu na
kuhakikisha vinawanufaisha kufikia
malengo yao ,bado
tutaendelea kushirikiana pamoja nanyi na jamii kwa ujumla katika kuhakikisha
tunatimiza lengo letu la kuboresha maisha ya watanzania kupitia huduma na
bidhaa zetu za kibunifu na fursa
za kibiashara’ aliongeza Singano.
Kwa upande wake mwenyekiti
wa Taasisi ya haki za binadamu na maendeleo ya kiuchumi kwa watu wenye ulemavu
Bw. Abubakar Rakesh alisema” tunayofuraha kuona baadhi ya wenzetu wakiwezeshwa
kupata rasilimali muhimu za kuanzisha biashara.
Tunawashukuru Airtel kwa
msaada huo na kwa kukiwezesha kikundi hiki kuwa cha kwanza kupata msaada kama
huu . Wito wangu kwa wanachama wenzangu ni kutumia nafasi hii vizuri, kuweka
jitihada katika kazi zao ili kufanya vyema na kufanikiwa katika biashara
zao”
“Napenda kutoa shukrani
zangu za pekee kwa serikali na kwa Mh Makamba,kwa mchango wake na kujitolewa
kwake kuwasaidia watu wenye ulemavu” aliongeza Rakesh
No comments:
Post a Comment