Rais wa Band ya FM Academia, Nyoshi El Saadat akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu tamasha la burudani liitwalo 'Beach
Band Bonanza' litakalofanyika kesho Jumamosi katika Ufukwe wa Azura, Kawe
jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja
Biashara wa Kampuni ya Mabibo Beer inayodhamini bonanza hilo kupitia kinywaji
cha Windhoek, Joseph Boniface.
Na Mwandishi Wetu
BENDI mbalimbali za muziki wa
dansi na wasanii wa Bongo Fleva wanatarajia kushiriki katika bonanza la
burudani liitwalo ‘Beach Band Bonanza’ litakalofanyika Desemba 20 katika Ufukwe wa
Azura, uliopo Kawe jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa
habari, Msemaji wa ‘Team Mamba’ ambao ni waratibu wa bonanza hilo, Doris
Godfrey alisema bonanza hilo litashirikisha bendi kama FM Academia ‘Wazee wa
Ngwasuma,’ Skylight, Mapacha Watatu, wasanii wa Bongo Fleva, akiwemo Dully
Sykes, CPWAA na Yamoto Band.
“Napenda kuwakaribisha katika
bonanza hili, tutachanganya ladha tofauti ili kuvutia kwa kujumuisha Bongo
Fleva na Dansi, kiingilio kitakuwa Sh 10,000 na watoto Sh 5,000, tunatarajia
kuanza saa sita mchana na pia kutakuwa na michezo mbalimnbali ya watoto,”
alisema.
Meneja Biashara wa Kampuni ya
Mabibo Beer inayodhamini bonanza kupitia kinywaji cha Windhoek, Joseph
Boniface, alisema bonanza hilo ni la aina yake na wao wameamua kuzikutanisha
bendi za muziki wa Dansi na Bongo Fleva kuwapa burudani mashabiki.
No comments:
Post a Comment