Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (Taswa), Amir Mhando akifafanua jambo kuhusu maandalizi ya hafla ya utoaji wa tuzo kwa wanamichezo bora wa mwaka ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein. Kushoto ni Mjumbe wa Tawsa, Mwani Nyangasa na Makamu Mwenyekiti wa Taswa, Egbert Mkoko. (Picha na Francis Dande)
Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar (SMZ), Dk. Ali Mohamed Shein, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
sherehe ya Tuzo za Wanamichezo Bora wa Mwaka, zinazoandaliwa na Chama cha
Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
Tuzo hizo zinatarajiwa
kufanyika kesho, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, ambapo jumla ya tuzo 46
zinatarajiwa kutolewa kwa wanamichezo mbalimbali, sambamba na Tuzo ya Heshima
ambayo ilitwaliwa kipindi kilichopita na Rais Mstaafu, Benjamin William Mkapa.
Akizungumza na waandishi wa
habari Jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Taswa, Egbert Mkoko
alisema, tuzo hizo zinatarajiwa kuwa za aina yake, ambazo zitatolewa sanjari na
pesa taslim kwa washindi.
Mkoko alisema, wanazingatia
mambo mbalimbali ili mtu aweze kuwa mshindi katika tuzo hizo, ambayo ni mchango
wa mchezaji husika katika timu yake pamoja na timu ya Taifa, nidhamu ya mchezaji
ndani na nje ya uwanja, uhusiano wake na jamii inayomzunguka, kipaji cha
kipekee kwa mchezaji husika.
Vigezo vingine walivyoangalia
ni awe mwamasishaji na mwenye ushawishi kwa wenzake, huku kigezo cha ziada,
mchezaji asiwe anatumia dawa zinazozuiliwa michezoni.
Aidha Mkoko alisema, kwa
upande wa burudani ambayo itaburudisha siku hiyo, bado wanaendelea na
mazungumzo na bendi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment