Mshindi wa shindano la Big Brother Africa msimu wa tisa, Idrisa Sultan ambaye ni Mtanzania (kushoto) akifurahia mara baada ya kutangazwa mshindi.
Mshindi wa shindano la Big Brother Africa msimu wa tisa, Idrisa Sultan ambaye ni Mtanzania akifurahia mara baada ya kutangazwa mshindi.
Mshindi wa shindano la Big Brother Africa msimu wa tisa, Idrisa Sultan ambaye ni Mtanzania akifurahia mara baada ya kutangazwa mshindi.
Mshindi wa shindano la Big Brother Africa msimu wa tisa, Idrisa Sultan ambaye ni Mtanzania (kushoto), akipokea mfano wa hundi ya dola za kimarekani 300,000 kutoka kwa Mkurugenzi wa M-Net Africa, Wangi Mba-Uzoukwu katika hafla iliyofanyika nchini Africa Kusini juzi usiku.
NA ANDREW CHALE
MSHIRIKI wa Tanzania
katika shindano la Big Brother Africa Hotshots, Idris Sultan amefanikiwa
kushinda kitita cha dola 300,000, akiwabwaga washiriki wenzake kutoka nchi
nane.
Katika fainali ya shindano hilo la msimu wa tisa
ililofanyika juzi usiku nchini Afrika Kusini, Idris aliweza kuwambwaga wengine
saba waliofika hadi hatua ya mwisho ya fainali.
Mshiriki huyo kutoka jijini Arusha, alipata ushindi huo
kutokana na kupigiwa kura nyingi kutoka nchi tano tofauti, hivyo kuwazidi
wenzake ambao waliishia kura tatu, mbili , moja huku wengine wakikosa
kabisa.
Idris anakuwa Mtanzania wa pili kunyakua taji hilo,
akitanguliwa na Richard Bezuidenhout ambaye alishinda katika msimu wa pili,
akifuata nyayo za Mwisho Mwampamba aliyeshika nafasi ya pili katika msimu
kwanza.
Mwampamba pia alipata nafasi ya kushiriki pia msimu wa tano
wa shindano hilo na kufanikiwa kuingia fainali, akiishia nafasi ya tano.
Kwa ushindi huo, Idris ameibuka na kitita cha dola 300,000
za Marekani sawa na sh. mil 500 za Tanzania.
Akizungumzia ushindi huo, Ofisa Mahusiano Mkuu wa kampuni ya
Multchoice Tanzania ambao ni wasambazaji
wa visambusi vya Dstv, Barbra Kambogi, alisema ni faraja kubwa kwa Watanzania.
“Tunampongeza Idris kwa kutuwakilisha vema Tanzania. Tuna
kila furaha na kwa sasa tupo katika mipango ya kumpokea ambapo tutawatangazia
watanzania wote siku hiyo ya kumpokea,” alisema Barbra.
Shindano hilo ambalo lilifikia tamati juzi usiku, limedumu
kwa miezi miwili sawa na siku 61, awali lilikuwa na washiriki 26 kutoka nchi
mbalimbali za Afrika kabla ya kuchujwa mmoja hadi mwingine hadi kubaki nane.








No comments:
Post a Comment