Fair Play.
Timu za Simba na Mwadui Utd zikiingia uwanjani wakati wa mchezo wa kirafiki iliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1. (Picha na Francis Dande)
Kocha wa Mwadui Utd, Jamhuri Kihwelu (kulia) akiwa na Kocha Msaidizi Amri Said 'Stam' (katikati) wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba imeshinda 3-1.
Kikosi cha Simba.
Benchi la ufundi la Simba.
Mashabiki waliofika uwanjani.
Benchi la ufundi la Mwadui.
Kikosi cha Mwadui Utd.
Beki wa Simba, Mohamed Hussein akimtoka mshambuliaji wa
Mwadui Utd, Salim Khamis wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ahmed Mkweche akimtoka mchezaji wa Simba.
Kipa wa Simba Ivo Mapunda akiokoa moja moja ya hatari langoni mwake huku akizongwa na mshambuliaji wa Mwadui Utd, Uhuru Selemani.
Wachezaji wa Simba wakishangilia ushindi wa timu yao.
Wachezaji wa Mwadui Utd wakishangilia bao lao la kufutia machozi.
Wachezaji wa Simba wakishangilia ushindi wa timu yao.
Wachezaji wa Mwadui Utd wakishangilia bao lao la kufutia machozi.
Wachezaji wa Simba wakitoka mapumziko.
Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu
TIMU
ya soka ya Simba leo imewatandika bakora 3-1 Mwadui Utd inayofundishwa na Kocha aliyewahi kuifundisha Simba, Jamhuri
Kihwelu ‘Julio’, kwa kuwabandika mabao 3-1 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa
Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Mechi
hiyo iliyokuwa yenye msisimko mkubwa kutokana na Mwadui Utd kuundwa na nyota
kadhaa waliowahi kung'ara wakati wakizichezea timu kubwa akiwemo Athuman Idd ‘Chuji,’ Uhuru
Selemani na Razak Khalfan, Ahmed Mkweche na Julius Mrope.
Mbali
ya nyota hao waliopangwa kikosi cha kwanza cha Mwadui, nyota wengine
mahiri kama Juma Jabu na BakarKigodeko, walikuwa katika benchi,
hivyo kuongeza mvuto wa mechi hiyo licha ya tofauti ya madaraja ya timu
hizo.
Dakika
ya 10, Simba walikuwa wa kwanza kufika katika lango la Mwadui Utd, mpira
uliopigwa na Iddy Bahati kutoka kushoto mwa lango na kukosa mmaliziaji.
Dakika
ya 22, Simba walifika kwa mara ya pili katika lango la Mwadui, lakini Ibrahim
Ajibu alishindwa kuitendea haki krosi-pasi murua ya Hassan Kessy aliyetua
Msimbazi kupitia usajili wa dirisha dogo akitokea Mtibwa Sugar ya Turiani,
Morogoro.
Dakika
ya 26, Simba walipata bao la kwanza likifungwa na Ibrahim Ajibu kabla ya vijana
wa Mwadui Utd kucharuka na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 30, likifungwa na
Salim Hamis.
Simba
walizidi kulisakama lango la Mwadui Utd na kufanikiwa kupata bao la pili dakika
37, likifumgwa kwa mara nyingine na Ajibu, hivyo Simba kwenda mapumziko wakiwa
mbele kwa mabao 2-1.
Kipindi
cha pili kiliendelea kuwa cha mashambulizi kwa kila upande, lakini Simba
wakionekana wametulia zaidi na kufanikiwa kupata bao la tatu likifungwa na Yusufu
Mbaraka akipokea pasi kutoka kwa beki mahiri Kessy aliyekuwa mwiba mkali akipanda
na kushuka.
No comments:
Post a Comment