Na Mwandishi Wetu
MKUGENZI wa Kituo cha Kulelea Watoto Yatima na
Wasiona (Chakuwama), Hassan Hamis, ameishauri jamii kujikita zaidi katika
kuwasidia watoto yatima ili kuwaepusha na ukosefu wa maadili pindi watakapokuwa
wakubwa.
Hamisi alisema hayo wakati kituo hicho kilichoko Sinza wilayani Kinondoni
jijini Dar es Salaam, kilipopokea msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vya
shule ikiwa ni msaada uliyotolewa na Shirika la Umeme nchini (Tanesco).
Alisema, kama watoto hao wataachwa bila msaada
wowote basi jamii itambue kuwa huenda taifa likapoteza viongozi bora na
kusababisha matatizo makubwa kwa watoto hao.
Hamisi, alisema kwa kulitambua hilo ndio maana
imeamua kuwakusanya watoto hao kwa kuwaweka pamoja na kuwapatia msaada
mbalimbali ikiwemo elimu.
“Kituo chetu kina watoto 60 na tunawapatia
huduma ya elimu ambayo ni muhimu katika taifa letu kwani tunaimani kuwa hapa
tutazalisha wataalamu na viongozi bora wa kesho,”alisema.
Pamoja na changamoto zinazokikabili kituo hicho
bado hawajakata tamaa hivyo wanashukuru inapotokea wadau wanapowapatia msaada
kama ililivyofanya Tanesco.
“Nashauri wadau wawasaidie watoto hawa na isiwe
katika kituo hiki tu bali katika vituo vyote vinavyojitolea kuwalea itakuwa
tumewaondolea matatizo yanayoweza kuwakabili watoto hao,”alisema Hamisi.
Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Dekland Mhaiki
alisema walifika katika kituo hicho ili kujionea maendeleo ya watoto hao pamoja
na changamoto zinazowakabili wanaamini watakaporudi tena watakuwa na ufumbuzi
katika kile walichokiona.
“Nimefarijika kuona maendeleo ya watoto hawa
katika kituo hiki na tumewapatia vifaa vya shule na vyakula vya aina mbalimbali
kama sehemu ya mgawo wetu,”alisema Mhaiki.


No comments:
Post a Comment