Na Happiness Katabazi, UB
MAKAMU wa Rais ,Dk.Mohammed Gharib Bilal Kesho anatarajiwa Kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekwaji wa jiwe la Msingi la Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), zitakazofanyika Jumamosi Januari 17 katika Kijiji cha Kiromo, Bagamoyo Mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Mikocheni
Dar es Salaam, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho anayeshughulikia
Fedha na Utawala, Dk.Elifuraha Mtalo alisema sherehe hizo zitafanyika
Katika Kijiji cha Kiromo na kwamba uwekwaji wa jiwe hilo ni ufunguzi
rasmi wa ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo Katika Kijiji hicho ambao
unatarajiwa kuanza Mwaka huu.
Dk.Mtalo alisema Dk.Bilal ndiye atakuwa mgeni rasmi pia
na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa naye anatarajiwa kuwa miongoni mwa wageni
walioalikwa katika sherehe hiyo ya kihistoria katika Wilaya ya Bagamoyo
kwasababu Somo la Historia linatufundisha kuwa mji wa Bagamoyo watumwa
walikuwa wakiishi.
" UB tunaifahamu historia ya Mji wa Bagamoyo ndiyo maana
tukaamua kuanzisha Chuo Kikuu ambacho tumekipa jina la University of
Bagamoyo.Kupitia Mji wa Bagamoyo tulikuwa watumwa, hivyo kupitia UB
ambayo inajenga makazi yake ya kudumu katika mji huo, binadamu wote
watakuwa huru kwasababu tutapata elimu" alisema Dk.Mtalo.
Alisema UB ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 2011 ambayo ina
makazi yake yake ya muda ,Mikocheni B, Dar es Salaam na kwamba ujenzi
wa Makazi ya kudumu ya UB kijijini Kilomo , utasaidia kukuza shughuli za
uchumi, wananchi wa eneo hilo kupata huduma ya elimu ya ngazi ya Chuo
Kikuu kwa ukaribu na ajira.
Aidha aliwaomba wananchi Wilaya Bagamoyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kujitokeza kwa Wingi Katika sherehe hiyo



No comments:
Post a Comment