HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 04, 2015

RAIS KIKWETE KUMUAPISHA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KESHO





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete anatarajiwa kumuapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya
Bwana George Mcheche Masaju (pichani) siku ya Jumatatu

Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

No comments:

Post a Comment

Pages