HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 17, 2015

AFRICAN SPORTS, MWADUI FC KUCHEZA FAINALI JUMAPILI

Timu za African Sports ya Tanga na Mwadui FC ya Shinyanga zinatarajiwa kucheza mchezo wa fainali ya kusaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) siku ya jumapili katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

African Sports waliibuka washindi wa kwanza katika Kundi A, na Mwadui FC washindi wa kwanza Kundi B watacheza mchezo huo wa fainali ambapo Bingwa atapewa zawadi ya Kombe na medali, hali kadhalika kwa msindi wa pili.

Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ilimalizika mwishoni mwa wiki kwa timu nne kupanda Ligi Kuu kwa kila kundi kutoa timu mbili, Kundi A ni African Sports na Majimaji FC, Kundi B ni timu za Mwadui FC na Toto Africans.

Nazo timu za Green Worriors na Villa Squad zimeteremka Daraja la pili baada ya kushika nafasi za mwisho kwenye msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza, Villa Squad kutoka Kundi A na Green Warriors Kundi B.

TFF YAZIPONGEZA AFRICAN SPORTS, MWADUI, MAJIMAJI NA TOTO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini – TFF Bw. Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Wenyekiti wa klabu ya African Sports (Tanga) , Majimaji (Ruvuma),  Mwadui (Shinyanga) na Toto Africans ya Mwanza kwa timu zao kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).

Katika salamu zake Bw. Malinzi amesema vilabu hivyo vinapaswa kujipanga na kufanya maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2015/2016, kwani VPL ni ngumu kutokana na timu zote kuwa na ushindani mkubwa wa kutafuta matokeo mazuri kuepeuka kushuka daraja.

Kwa niaba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini -TFF, familia ya mpira na watanzania kwa ujumla wanawapa pongezi timu za African Sports, Majimaji, Mwadui na Toto Africans kwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom na kuwatakia maandalizi mema ya VPL 2015/2016.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments:

Post a Comment

Pages