HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 28, 2015

Bayport yaguswa na mauaji ya albino Tanzania

 Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir akizungumza na Ester Jonas, aliyelazwa Hospitali ya Bugando aliyejeruhiwa kufuatia tukio la uporwaji wa mtoto wake Yohana Bahati. Kulia kwa Mbunge ni Meneja Mauzo wa Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala, akiwa na watumishi wengine wa taasisi hiyo jijini Mwanza.

 NA MWANDISHI WETU, MWANZA


 TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services yenye makao yake Makuu jijini Dar es Salaam, imeguswa na kukemea vikali mauaji ya albino yanayoendelea kutokea nchini, huku ikifunga safari hadi wilayani Misungwi kutembelea familia ya Pendo Emmanuel, albino aliyeporwa Desemba 27, katika kijiji cha Ilelema, wilayani Chato, mkoani Geita na hajulikani
alipokuwa hadi leo.
Ustawi wa Jamii Mwanza, Leah Linti, Katibu Tawala Msaidizi Crecencia Joseph, Mweka Hazina wa Chama cha Albino Taifa(TAS), AbdullahOmari, Jeshi la Polisi wilayani Misungwi, huku safari zotezikiwa chini ya uangalizi wa Mkuu wa Mkoa 

Katika ziara hiyo, Bayport waliambatana na Mbunge wa Viti
Maalum, Al Shaimar Kweigyir, huku wakiiwezesha kwa kiasi
kikubwa safari, iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya kutoa pole
kwa familia ya Pendo na ya Yohana Bahati, albino aliyeuawa kijiji cha mkoani Mwanza.

 Safari hiyo ilianzia katika Hospitali ya Bugando Mwanza,
kumtembelea Ester Jonas, ambaye ni mama wa Yohana Bahati anayetibiwa hospitalini ambapo alikabidhiwa Sh Milioni 2 kwa ajili ya kusimamia afya yake
pamoja na mahitaji yake mengine ya kijamii.

Baada ya kukabidhi kiasi hicho cha pesa, Mbunge aliambatana
na viongozi wa Bayport Mwanza na wadau wengine kwenda
kutembelea familia ya Pendo, ambapo pia alipewa Sh Milioni


Akizungumza katika safari hiyo, Mbunge Shaimar alisema
ameendelea kusikitishwa na mauaji hayo ya albino yanayotoa
haki ya kuishi ya watu wote wenye ulemavu wa ngozi.

Alisema mauaji hayo yanawafanya albino waishi kwa mashaka
katika nchi zao, jambo linalohitaji nguvu ya ziada kupambana
na watu wote wenye vitendo viovu vya kuwadhuru wenye ulemavu
wa ngozi.

 “Naumia juu ya vitendo hivi kwasababu na mimi nipo kwenye
kundi hili lawatu wenye ulemavu wa ngozi wanaoendelea
kupukutika siku hadi siku, hivyo tupambane na majangili haya, maana najua Mheshimiwa Rais, Dr Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wamekuwa wakiguswaa mno
na matukio haya yanayoichafua nchi yetu.

 “Nimeamua kuambatana na marafiki zangu, wakiwamo Bayport
Financial Services na kukabidhi kiasi kidogo cha pesa
pamoja  na mafuta ya kupaka ya watu wenye ulemavu wa
ngozi kwa mama wa Pendo na Yohana, ambao bado wana watoto wenye ulemavu wa ngozi,”
alisema.

Naye Meneja Mauzo wa Bayport Financial Services Kanda ya
Ziwa, Lugano Kasambala, alisema wananchi na serikali
waendelee kupambana ili kulinda haki ya kuishi ya watu wenye
 ulemavu wa ngozi wanaoendelea kuangamia kila wakati sehemu mbalimbali za nchi yetu.

 “Sisi Bayport Financial Services tumeamua kuambatana na
mbunge Shaimar ili kujionea hali hii pamoja na kushiriki
naye kwa kiais kikubwa kamaa balozi wa watu wenye ulemavu wa
ngozi, huku tukiaminikuwa mwendo huu utaambatana na kutoa elimu kwa wote ili tulinde haki za albino Tanzania.

“Hata hivyo juhudi za ulinzi zinahitajika kwa sababu maeneo wanayoishi hawa ndugu zetu, hususan vijijini nihatari, hali inayoweza kuwafanya waishi kwa mashaka dhidi ya  majangili hao wanaojidanganya kwamba viungo vya albino ni njia ya kuwapatia utajiri, wakati si kweli,” alisema Kasambala.

Wengine waliombatana kwenye ziara hiyo ni pamoja na Afisa
wa Mwanzaa, Magesa Mulongo.

No comments:

Post a Comment

Pages