HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 18, 2015

Msama kumwaga baiskeli 100

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusiana na maandalizi ya tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 5 kwenye Uwanja wa Taifa. Sehemu ya mapato ya tamasha hilo yatatumika kununulia baiskeli 100 kwa ajili ya watu wenye ulemavu. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusiana na maandalizi ya tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 5 kwenye Uwanja wa Taifa. Sehemu ya mapato ya tamasha hilo yatatumika kununulia baiskeli 100 kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusiana na maandalizi ya tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 5 kwenye Uwanja wa Taifa. Sehemu ya mapato ya tamasha hilo yatatumika kununulia baiskeli 100 kwa ajili ya watu wenye ulemavu.

NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam inayoratibu tamasha la Pasaka ambalo mwaka huu linatarajiwa kutikisa mikoa 17, imepanga kutumia sehemu ya fedha za kiingilio kununua baiskeli 100 kwa ajili ya kusaidia watu wenye ulemavu.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Alex Msama wakati akielezea maandalizi ya Tamasha hilo ambalo litakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 15 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000 katika kuutangaza utukufu wa Mungu. 

Alisema baiskeli hizo 100 zitagawanywa katika mikoa 10 na kutoa wito kwa wadau wa muziki wa injili kujitokeza kwa wingi katika mikoa mbalimbali ambako tamasha hilo litafanyika likipambwa na waimbaji mahiri kutoka ndani na nje ya nchi.

Msama alisema utoaji wa baiskeli hizo za walemavu ni mwendelezo wa moja ya malengo ya tamasha hilo ambapo ni kusaidia makundi maalumu katika jamii na kuongeza baada ya hapo kufanikisha hili, wataangalia nini wafanye dhidi ya makundi mengine.

Kuhusu waimbaji, Msama amesema kamati yake kwa sasa ipo katika hatua ya mwisho ya mazungumzo na waimbaji mbalimbali wa kimataifa hasa kutoka nchini Afrika Kusini na Uingereza ambako mazungumzo yanakwenda vizuri.

Aliwataja waiombaji wanaofanya nao mazungumzo ni Solly Mahlangu, Rebecca Malope, Kekeletso Foofolo na wengineo kutoka nchini humo kwa lengo la kuja kupamba tukio hilo la maadhimisho ya miaka 15 ya Tamasha la Pasaka.

Msama aliongeza kuwa, hadi sasa wamepata maombi ya mikoa 17 wakitaka tamasha hilo liwafikie, hivyo wanachoafanya sasa ni kufanya uchambuzi kuona mikoa gani wanaweza kuifikia kulingana na sababu mbalimbali ikiwemo mazingira halisi ya kijiografia na kifedha.

“ Hoja si kupendekezwa au kuombwa tu na wadau, lazima tuangalie na mazingira ya mkoa husika katika mambo ya matamasha,” alisema Msama.
Aliitaja mikoa iliyoomba Tamasha hilo ni Morogoro, Rukwa,  Mara, Singida, Arusha, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Tanga, Dar s Salaam, Mtwara, Mwanza, Dodoma, Tabora, Shinyanga, Kilimanjaro na Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Pages