HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 02, 2015

RAIS KIKWETE AONGOZA MAELFU YA WAOMBOLEZAJI KATIKA KUAGA MWILI WA KAPTENI JOHN KOMBA

 Askari wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Komba wakati wa kuaga mwili wake katika viwanja vya Karimee jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Francis Dande)
Jeneza la Kapteni John Komba
Rais Jakaya Kikwete (wa tatu kushoto) akiwaongoza viongozi mbalimbali wakati wa kuaga mwili wa Mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu John Komba. 
 Wanafamilia.
Salome Komba (kushoto) mke wa Kapteni John Komba akiwa na wanafamilia wengine. 
 Umati wa watu ukiwa katika viwanja vya Karimjee wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Kapteni Komba.
 Waombolezaji wakinunua kanga zilizobeba ujumbe mahsusi katika msiba wa Mh. Komba.
Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.
Viongozi mbalimbali wakiwa katika katika msiba wa Komba.
 Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (kushoto) akiwa na mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi (katikati) akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (kushoto) na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu.
 Umati wa watu wakiwa katika foleni ya kwenda kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba mbunge wa Mbinga Magharibi.
Wasanii wa bongo fleva wakiimba wimbo maalum.
 Rais Jakaya Kikwete akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Komba. 
 Rais Kikwete akitoa heshima za mwisho.
Rais Kikwete akitoa heshima za mwisho.
Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal na wake zake Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Kapteni John Komba. 
 Mbunge wa Monduli akitoa heshima za mwisho.
 Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba akilia kwa uchungu mara baada ya kutoa heshima za mwisho.
 Spika wa Bunge Anne Makinda akitoa heshima za mwisho.
 James Mbatia akitoa heshima za mwisho.
 Mkurugenzi Mtendaji wa IPP, DK. Reginald Mengi akipita mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa Kapteni John Komba.
 Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa akitoa salama za mwisho.
 Mbunge wa Vunjo Agustino Lyatonga Mrema akitoa heshima za mwisho.
 Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa (wa pili kulia) akitoa heshima za mwisho.
Umati wa watu ukitaka kutoa heshima za mwisho.
 Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbroad Slaa akiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jaji Damian Lubuva katika msiba wa Kapteni John Komba.
Rais mstaafu Benjamin Mkapa akiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Na Mwandishi Wetu


RAIS Jakaya Kikwete leo wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa Mbunge wa Mbinga Magharibi Kepteni John Komba, amejikuta kububujikwa na machozi baada ya wasanii wa muziki wa dansi wakiongozwa na mwanamuzii mkongwe King Kiki kuimba umbo wa ‘Nani Yule’
Rais Jakaya Kikwete akifuta machozi.
Rais Jakaya Kikwete akilia baada ya kusikia wimbo maalum wa maombolezo ujulikanao kwa jina la 'Nani Yule'.
 
Wimbo maalumu wa maombolezo uliyomliza Rais Kikwete ni ule ujulikanao kwa jina la ‘Nani Yule’ ambao uliimbwa na kikundi cha muziki wa dansi.

Rais Kikwete alijikuta katika hali hiyo baada ya msanii Jose Mara kuimba wimbo huo kwa hisia kali.

Nyimbo nyingine ulikuwa ni ule ulioimbwa na msanii Ruby na watatu ulimbwa na wasanii wa muziki wa Bongo Fleva na Bongo Move.
Ukiachilia mbali Rais Kikwete kulia, pia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, ambaye alilia huku akisema kuwa chama hicho kimepoteza jino la dhahabu na kubaki na pengo ambalo haliwezi kuzibika tena.

Awali katika maombolezo hayo ya kutoa heshima za mwisho kwa Kepteni Komba, ndugu, jamaa na wananchi walianza kuwasili katika viwanja vya Karimjee majira ya 4:00 hadi 4:30 Asubuhi.

Wengine waliowasili walikuwa viongozi wa vyama vya Siasa, wabunge, Manaibu Mawaziri, Mawaziri ambapo wote walipofika waliketi katika maeneo waliko pangiwa huku kila mmoja akitafakari msiba huo.
Joshua Nasari Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema).
Aidha Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni alitakiwa kufika majira ya saa 4:33 asubuhi hata hivyo kiongozi huyo hakuweza kufika kutokana na kuwa safarini, baadala yake aliwakilishwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari. 
Spika wa Bunge Anne Makinda
Naye Spika wa Bunge, Makinda aliwasili majira ya saa 4:39 asubuhi ambapo Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilali alifika saa 4:50 asubuhi.

Ilipotimia saa 5:15 asubuhi, Rais Jakaya Kikwete, aliwasili kitika viwanja hivyo vya Karimjee huku akiambatana na mke wake Salma.

Mara baada ya kufika Rais, mwili wa mrehemu nao uliwasili katika viwanja hivyo huku ukiandamana na familia ya marehemu pamoja na ndugu wa karibu na majirani.

Baada ya viongozi mbalimbali, wakuu wa Idara za Ofisi za Serikali pamoja na wanchi, viwanja hivyo vya karimjee vilifurika umati mkubwa wambolezaji hao.

Hata hivyo, uwepo wa baadhi ya viongozi kutoka idara, taasisi mashirika ya kiserikari inaelezwa kwamba huduma nyingi zilisimama kwa ajili ya watendaji wake kwenda kutoa heshima za mwisho. 

Huku wakiwa katika huzuni na majonzi baadhi ya waombolezaji walishindwa kujizuia kwani waliangua kilio pale mwili huo ulipowasili katika viwanja hivyo.

Sala fupi

Baada ya mwili wa marehemu kuwasili ilifanyika sala fupi iliyoendeshwa na Padre wa Kanisa la Kikatoliki, Parokia ya Bikira Maria, Frowi Tindwi.

Wananchi wa nena

Wananchi walionesha wasiwasi kuhusu utendaji kazi wa Shirika la Utangazaji katika kuripoti taarifa za msiba huo wakwani hawakuupa kipaumbele, wakishindwa kutoa ratiba kamili hali iliyowafanya baadhi ya wananchi kushindwa kujua muda na wapi yalikuwa yanafanyika.

Kituko
Katika hali isiyo ya kawaida wapiga picha kutoka vyombo mbalimbali vya habari walijengewa uzio, uliyowafanya washindwe kufanya kazi zao kwa uhuru.

Hali hiyo iliwafanya washindwe kupata sura za wahusika na baadala yake kupata upande wa nyuma wa mwili, kadhia hiyo iliendelea hadi pale Rais Kikwete, alipoagiza waandishi hao waachiwe ili wapige picha katika pembe inayowafaa.

Rais Kikwete baada ya kutoa heshima za mwisho, alitia saini Kitabu cha Maombolezo ya Kepteni Komba, ambaye alifariki dunia Jumamosi Februari 28 mwaka huu kwenye Hospitali ya TMJ,ambako alikimbizwa ili kupata matibabu ya ugonjwa wa Kisukari.
Baada ya waombolezaji kuuaga mwili huo wa marehemu kulingana na Itifaki uliondolewa katika viwanja hivyo kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julus Nyerere (JNIA).

Ratiba

Majira ya saa 8:00 mchana Mwili wa marehemu ukiambatana na familia pamoja na waombolezaji, uliondoka katika viwanja vya Karimjee kuelekea Songea ambapo utapokelewa na Mkuu wa Mkoa.

Ratiba hiyo inaonesha kuwa baada ya mwili huo kupokelewa, majira ya saa 10:00 hadi 10:15 alaasiri, utapelekwa katika uwanja wa Majimaji ambako wananchi wite watapata fursa ya kutoa heshima yao ya mwisho.

Baada ya kutoa heshima hiyo ya mwisho 10:115 hadi saa 11:00 jioni utapelekwa Kijijini kwake Lituhi Nyasa kwa ajili ya mazishi leo.


No comments:

Post a Comment

Pages